< 2 Wathesalonike 2 >

1 Sasa yahusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa kwetu pamoja tukae naye. Ndugu, tunawaombeni sana
But as to the coming of our Lord Jesus Christ, and our gathering together unto Him,
2 msifadhaike upesi moyoni, na wala msitiwe wasiwasi kwa sababu ya madai kwamba Siku ya Bwana imekwisha fika. Labda inadhaniwa kwamba jambo hili limetokana na uaguzi fulani, mahubiri au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu.
we beseech you, brethren, that ye be not soon moved from your steadiness of mind, or troubled, neither by Spirit, nor by word, nor by letter, as from us, that the day of Christ is at hand.
3 Msikubali kudanganywa na mtu yeyote kwa namna yoyote ile. Maana Siku hiyo haitakuja mpaka kwanza ule Uasi Mkuu utokee na yule Mwovu aonekane ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa.
Let not any one deceive you by any means; for it shall not come till there come an apostasy first, and the man of sin be revealed,
4 Yeye atapinga kila kitu wanachokiona watu kuwa ni mungu, au wanachokiabudu. Naam, hata ataingia na kuketi ndani ya Hekalu la Mungu akijidai kuwa Mungu.
the son of perdition, who opposeth and exalteth himself above all that is called God, or the object of worship; so that he sits as God in the temple of God, shewing himself that he is God.
5 Je, hamkumbuki kwamba niliwaambieni haya yote wakati nilipokuwa pamoja nanyi?
Do ye not remember, that when I was with you, I told you these things?
6 Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
And ye know what now hindereth him from being revealed in his own time.
7 Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
For the mystery of iniquity is already working, only there is one that hindreth till he be taken out of the way.
8 Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng'ao wa kuja kwake.
And then the wicked one shall be detected, whom the Lord will destroy by the breath of his mouth, and abolish by the brightness of his coming:
9 Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
who comes, through the efficacy of Satan, with all kind of lying power, and signs,
10 na kutumia udanganyifu wa kila namna kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea. Hao watapotea kwa sababu hawakuupokea na kuupenda ule ukweli ili waokolewe.
and wonders, and with all iniquitous fraud, among those that shall perish; because they received not the love of the truth, by which they might be saved.
11 Ndiyo maana Mungu amewaweka chini ya nguvu ya upotovu, wauamini uongo.
And for this cause God will send upon them the efficacy of error, so that they shall themselves believe the lie:
12 Matokeo yake ni kwamba wote wasioamini ukweli, ila wafurahia dhambi, watahukumiwa.
that they may all be condemned, who believed not the truth, but had pleasure in iniquity.
13 Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu, ninyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
But we ought always to give thanks to God for you, brethren beloved of the Lord; because God hath from the beginning chosen you to salvation, through sanctification of the Spirit, and belief of the truth:
14 Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni; aliwaiteni mpate kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
to which He hath called you by our gospel, to the obtaining of the glory of our Lord Jesus Christ.
15 Basi, ndugu, simameni imara na zingatieni yale mafundisho tuliyowafundisheni kwa mahubiri yetu na barua zetu.
Therefore, brethren, be steady, and hold fast the traditions, which ye have been taught, whether by word or by our letter.
16 Tunamwomba Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu ambaye alitupenda, na kwa neema yake akatujalia faraja ya milele na tumaini jema, (aiōnios g166)
And may our Lord Jesus Christ himself, and our God and Father, who hath loved us, and hath given us everlasting consolation, and good hope through grace, comfort your hearts, (aiōnios g166)
17 aifariji mioyo yenu na kuwaimarisheni ili mweze daima kutenda na kusema yaliyo mema.
and establish you in every good word and work.

< 2 Wathesalonike 2 >