< 2 Wakorintho 4 >

1 Basi, Mungu, kwa huruma yake, ametukabidhi kazi hii na hivyo hatufi moyo.
Therefore, since we have this ministry through God's mercy, we do not lose heart.
2 Tumeyaacha kabisa mambo yote ya aibu na ya kisirisiri. Hatuishi tena kwa udanganyifu, wala kwa kulipotosha neno la Mungu; bali tunaudhihirisha ukweli kwa kuufanya ukweli, na hivyo kujiweka chini ya uamuzi wa dhamiri za watu mbele ya Mungu.
Rather, we have renounced shameful hidden deeds; we do not act deceitfully or distort the word of God, but by openly proclaiming the truth we commend ourselves to everyone's conscience in the sight of God.
3 Maana, kama Habari Njema tunayohubiri imefichika, imefichika tu kwa wale wanaopotea.
But even if our gospel is veiled, it is veiled among those who are perishing.
4 Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu. (aiōn g165)
The god of this age has blinded the minds of unbelievers like them, so that the light of the gospel of the glory of Christ, who is the image of God, might not dawn upon them. (aiōn g165)
5 Maana hatujitangazi sisi wenyewe, ila tunamhubiri Yesu Kristo aliye Bwana, sisi wenyewe tukiwa watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
For what we preach is not ourselves, but Christ Jesus as Lord, and ourselves as your servants for Jesus' sake.
6 Mungu ambaye alisema, “Mwanga na uangaze kutoka gizani,” ndiye mwenye kuiangaza mioyo yetu, na kutupatia mwanga wa ujuzi wa utukufu wa Mungu uangazao katika uso wa Kristo.
For God, who commanded light to shine out of darkness, has shone in our hearts to give us the light of the knowledge of the glory of God in the face of Jesus Christ.
7 Basi, sisi tulio na hazina hii tuko tu kama vyombo vya udongo, ili ionekane wazi kwamba nguvu hiyo kuu yatoka kwa Mungu wala si kwetu sisi wenyewe.
But we have this treasure in jars of clay, to show that this extraordinary power is from God and not from us.
8 Daima twapata taabu, lakini hatugandamizwi; twapata mashaka, lakini hatukati tamaa;
We are afflicted in every way, but not crushed; perplexed, but not in despair;
9 twateseka, lakini hatuachwi bila msaada; na ingawa tumeangushwa chini, hatukuangamizwa.
persecuted, but not forsaken; struck down, but not destroyed;
10 Kila wakati tumekuwa tukichukua mwilini mwetu kifo cha Kristo, ili uhai wake Yesu pia udhihirike katika miili yetu.
always carrying about in our bodies the death of the Lord Jesus, so that the life of Jesus may also be revealed in our bodies.
11 Naam, katika maisha yetu yote tunakabiliwa na kifo daima kwa ajili ya Yesu, ili uzima wake Yesu udhihirike katika miili yetu inayokufa.
For we who live are always being delivered up to death for Jesus' sake, so that the life of Jesus may also be revealed in our mortal flesh.
12 Hii ina maana kwamba ndani yetu kifo kinafanya kazi, lakini ndani yenu uhai unafanya kazi.
So then, death is at work in us, but life is at work in you.
13 Maandiko Matakatifu yasema: “Niliamini, ndiyo maana nilinena.” Nasi pia, tukiwa na moyo huohuo wa imani, tunaamini, na kwa sababu hiyo twanena.
It is written, “I believed, therefore I spoke.” With that same spirit of faith we also believe, therefore we also speak.
14 Tunajua kwamba yule aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua sisi pia pamoja na Yesu na kutuweka mbele yake pamoja nanyi.
For we know that he who raised the Lord Jesus will also raise us through Jesus and bring us with you into his presence.
15 Yote haya ni kwa faida yenu; ili kama vile neema ya Mungu inavyoenea kwa watu wengi zaidi na zaidi vivyo hivyo watu wengi zaidi watoe shukrani nyingi kwa utukufu wa Mungu.
All of this is for your benefit, so that grace, as it extends to more and more people, may cause thanksgiving to abound to the glory of God.
16 Kwa sababu hiyo hatufi moyo; na hata kama maumbile yetu ya nje yataoza, lakini kwa ndani tunafanywa wapya siku kwa siku.
Therefore we do not lose heart. Even though on the outside we are wasting away, on the inside we are being renewed day by day.
17 Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu: lakini itatupatia utukufu upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho. (aiōnios g166)
For our light and momentary affliction is bringing about for us an eternal weight of glory far beyond all measure, (aiōnios g166)
18 Hivyo tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyoonekana ni vya muda tu; lakini vile visivyoonekana ni vya milele. (aiōnios g166)
as we look not to what is seen, but to what is unseen. For what is seen is temporary, but what is unseen is eternal. (aiōnios g166)

< 2 Wakorintho 4 >