< 2 Wakorintho 11 >

1 Laiti mngenivumilia kidogo, hata kama mimi ni mjinga kiasi fulani! Naam, nivumilieni kidogo.
I wish ye would bear with me a little in my folly; and indeed bear with me.
2 Ninawaoneeni wivu lakini ni wivu wa Mungu; maana ninyi ni kama bikira safi niliyemposa kwa mwanamume mmoja tu ambaye ndiye Kristo.
For I am jealous over you with a godly jealousy, having espoused you to one husband, that I may present you as a chaste virgin to Christ.
3 Lakini naogopa kwamba, kama vile yule nyoka kwa hila zake za uongo alimdanganya Hawa, fikira zenu zaweza kupotoshwa, mkauacha uaminifu wenu wa kweli kwa Kristo.
But I fear least as the serpent seduced Eve by his subtilty, so your minds should be corrupted from the purity that is in Christ.
4 Maana mtu yeyote ajaye na kumhubiri Yesu aliye tofauti na yule tuliyemhubiri, ninyi mwampokea kwa mikono miwili; au mnakubali roho au habari njema tofauti kabisa na ile mliyopokea kutoka kwetu!
For if he, that cometh to you, preacheth another Jesus, whom we have not preached; or if ye receive another Spirit which ye have not received, or another gospel which ye have not embraced, ye might indeed bear with him.
5 Sidhani kwamba mimi ni mdogo kuliko hao “mitume wakuu.”
For I think I was not inferior to the very chiefest apostles: and if I am unskilled in speech,
6 Labda sina ufasaha wa lugha, lakini elimu ninayo; jambo hili tumelionyesha wazi kwenu, kila mahali na kila wakati.
yet not in knowledge ---but we have been fully manifested among you in all things.
7 Mimi niliihubiri kwenu Habari Njema ya Mungu bila kudai mshahara; nilijinyenyekeza ili nipate kuwakweza ninyi. Je, nilifanya vibaya?
Have I committed an offence in humbling myself that ye might be exalted? and in that I have preached the gospel of God to you gratis?
8 Nilipofanya kazi kati yenu, mahitaji yangu yaligharimiwa na makanisa mengine. Kwa namna moja au nyingine niliwapokonya wao mali yao nipate kuwatumikia ninyi.
I trespassed on other churches, receiving maintenance from them for your service.
9 Nilipokuwa nanyi sikumsumbua mtu yeyote nilipohitaji fedha; ndugu waliotoka Makedonia waliniletea kila kitu nilichohitaji. Nilikuwa mwangalifu sana nisiwe mzigo kwa namna yoyote ile, na nitaendelea kufanya hivyo.
And when I was present among you, and in want, I was chargeable to no one. For the brethren that came from Macedonia supplied my want: and in every thing I have kept myself from being burdensome to you, and so I will keep myself.
10 Naahidi kwa ule ukweli wa Kristo ulio ndani yangu, kwamba hakuna kitakachoweza kunizuia kujivunia jambo hilo popote katika Akaya.
As the truth of Christ is in me, this boast shall not be taken from me in the regions of Achaia.
11 Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu eti siwapendi ninyi? Mungu anajua kwamba nawapenda!
Wherefore? because I love you not?
12 Nitaendelea kufanya kama ninavyofanya sasa, ili nisiwape nafasi wale wanaotafuta nafasi, nafasi ya kujivuna kwamba eti wanafanya kazi kama sisi.
God knoweth. But what I do, I will do, that I may cut off occasion from those that desire an occasion of boasting or censure, that in what they boast of they may be found to do even as we do.
13 Maana, hao ni mitume wa uongo, wafanyakazi wadanganyifu wanojisingizia kuwa mitume wa Kristo.
For such are false apostles, deceitful workers, transformed into apostles of Christ.
14 Wala si ajabu, maana hata Shetani mwenyewe hujisingizia kuwa malaika wa mwanga!
And no wonder: for Satan himself is transformed into an angel of light.
15 Kwa hiyo si jambo la kushangaza ikiwa na hao watumishi wake wanajisingizia kuwa watumishi wa haki. Mwisho wao watapata kile wanachostahili kufuatana na matendo yao.
It is therefore no great thing, if his ministers also be transformed into ministers of righteousness; whose end shall be according to their works.
16 Tena nasema: Mtu asinifikirie kuwa mpumbavu. Lakini kama mkifikiri hivyo, basi, nichukueni kama mpumbavu ili nami nipate kuwa na cha kujivunia angaa kidogo.
I say again, let no one think me foolish herein; but if they do, yet bear with my weakness, that I also may boast a little.
17 Ninachosema sasa si kile alichoniagiza Bwana; kuhusu jambo hili la kujivuna, nasema tu kama mtu mpumbavu.
What I speak I speak not as from the Lord, but as in weakness, in this confidence of boasting.
18 Maadam wengi hujivuna kwa sababu za kidunia, nami pia nitajivuna.
Since many boast in the flesh, I will boast also.
19 Ninyi ni wenye busara, ndiyo maana hata mnawavumilia wapumbavu!
For ye bear with fools willingly, being yourselves so wise:
20 Mnamvumilia hata mtu anayewafanya ninyi watumwa, mtu mwenye kuwanyonya, mwenye kuwakandamiza, mwenye kuwadharau na kuwapiga usoni!
ye bear it, even if any one enslave you, if any devour you, if any take your substance, if any be lifted up, yea if any one smite you on the face.
21 Kwa aibu nakubali kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Iwe iwavyo, lakini kama kuna mtu yeyote anayethubutu kujivunia kitu—nasema kama mtu mpumbavu—mimi nathubutu pia.
I speak of their reproaches, as if we were weak: but whereinsoever any one may be confident (though I speak foolishly) I may be confident too.
22 Je, wao ni Waebrania? Hata mimi. Je, wao ni Waisraeli? Hata mimi. Wao ni wazawa wa Abrahamu? Hata mimi.
Are they Hebrews? so am I: are they Israelites? so am I: are they the seed of Abraham?
23 Wao ni watumishi wa Kristo? Hata mimi—nanena hayo kiwazimu—ni mtumishi wa Kristo zaidi kuliko wao. Mimi nimefanya kazi ngumu zaidi, nimekaa gerezani mara nyingi zaidi, nimepigwa mara nyingi zaidi na nimekaribia kifo mara nyingi.
so am I: are they ministers of Christ? (if I may speak as a fool) I am more: in labors more abundant, in stripes far exceeding, in prisons more frequently, and often even in deaths.
24 Mara tano nilichapwa vile viboko thelathini na tisa vya Wayahudi.
From the Jews I have five times received forty stripes save one.
25 Nilipigwa viboko mara tatu, nilipigwa mawe mara moja; mara tatu nilivunjikiwa meli baharini, na humo nikakesha usiku kucha na kushinda mchana kutwa.
Thrice I have been beaten with rods, once I was stoned, thrice I have been shipwrecked, and was a night and a day on the deep:
26 Kila mara safarini nimekabiliwa na hatari za mafuriko ya mito, na hatari za wanyama; hatari kutoka kwa wananchi wenzangu na kutoka kwa watu wa mataifa mengine; hatari za mjini, hatari za porini, hatari za baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo
in journies often, in perils from rivers, in perils from robbers, in perils from my own nation, in perils from the heathen, in perils in the city, in perils in the desert, in perils on the sea, in perils among false brethren:
27 Nimefanya kazi na kutaabika, nimekesha bila usingizi mara nyingi; nimekuwa na njaa na kiu; mara nyingi nimefunga na kukaa katika baridi bila nguo.
in labor and toil, in watchings often, in hunger and thirst, in fastings often, in cold and nakedness: and beside these outward troubles,
28 Na, licha ya mengine mengi, kila siku nakabiliwa na shughuli za makanisa yote.
that which besets me daily, the care of all the churches.
29 Kama mtu yeyote ni dhaifu, nami pia ni dhaifu; mtu yeyote akikwazwa, nami pia huwa na wasiwasi.
Who is infirm, and I am not infirm also? who is offended, and I am not inflamed?
30 Ikinilazimu kujivuna, basi, nitajivunia udhaifu wangu.
If I must boast, I will boast of the things which relate to my infirmity.
31 Mungu na Baba wa Bwana Yesu—jina lake litukuzwe milele—yeye anajua kwamba sisemi uongo. (aiōn g165)
And the God and Father of our Lord Jesus Christ, who is blessed for ever, knoweth that I lye not. (aiōn g165)
32 Nilipokuwa Damasko, mkuu wa mkoa, aliyekuwa chini ya mfalme Areta, alikuwa akiulinda mji wa Damasko ili apate kunikamata.
In Damascus the governor under king Aretas, placed guards about the city to seize me:
33 Lakini, ndani ya kapu kubwa, niliteremshwa nje kupitia katika nafasi ukutani, nikachopoka mikononi mwake.
and I was let down by the wall through a window in a basket, and so escaped his hands.

< 2 Wakorintho 11 >