< 1 Timotheo 4 >
1 Roho asema waziwazi kwamba siku za baadaye watu wengine wataitupilia mbali imani; watazitii roho danganyifu na kufuata mafundisho ya pepo.
Now the Spirit speaketh expressly, that in the latter times some shall depart from the faith, giving heed to seducing spirits, and doctrines of demons;
2 Mafundisho ya namna hiyo yanaenezwa na watu waongo wadanganyifu, ambao dhamiri zao ziko kama zimechomwa kwa chuma cha moto.
Speaking lies in hypocrisy; having their conscience seared with a hot iron;
3 Watu hao hufundisha kwamba ni makosa kuona na pia kula vyakula fulani. Lakini Mungu aliviumba vyakula hivyo, ili wale walio waumini na ambao wanapata kuujua ukweli, wavitumie kwa shukrani.
Forbidding to marry, and commanding to abstain from meats, which God hath created to be received with thanksgiving by them who believe and know the truth.
4 Kila kitu alichoumba Mungu ni chema, wala hakuna kinachohitaji kukataliwa, bali vyote vipokelewe kwa sala ya shukrani,
For every creature of God is good, and nothing to be refused, if it is received with thanksgiving:
5 kwa sababu neno la Mungu na sala hukifanya kitu hicho kikubalike kwa Mungu.
For it is sanctified by the word of God and prayer.
6 Kama ukiwapa ndugu wote maagizo haya, utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, ukijiendeleza kiroho kwa maneno ya imani na mafundisho ya kweli, ambayo wewe umeyafuata.
If thou shalt put the brethren in remembrance of these things, thou shalt be a good minister of Jesus Christ, nourished by the words of faith and of good doctrine, to which thou hast attained.
7 Lakini achana na hadithi zile zisizo za kidini na ambazo hazina maana. Jizoeshe kuishi maisha ya uchaji wa Mungu.
But refuse profane and old wives’ fables, and exercise thyself rather to godliness.
8 Mazoezi ya mwili yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana yanatuahidia uzima katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
For bodily exercise profiteth little: but godliness is profitable to all things, having promise of the life that now is, and of that which is to come.
9 Usemi huo ni wa kusadikika kabisa na unastahili kukubaliwa.
This is a faithful saying and worthy of all acceptation.
10 Sisi tunajitahidi na kufanya kazi kwa bidii kwani tumemwekea tumaini letu Mungu aliye hai ambaye ni Mwokozi wa watu wote, na hasa wale wanaoamini.
For therefore we both labour and suffer reproach, because we trust in the living God, who is the Saviour of all men, especially of those that believe.
11 Wape maagizo hayo na mafundisho hayo.
These things command and teach.
12 Usikubali mtu yeyote akudharau kwa sababu wewe ni kijana, lakini jitahidi uwe mfano kwa wanaoamini: katika usemi wako, mwenendo wako, upendo, imani na maisha safi.
Let no man despise thy youth; but be thou an example of the believers, in word, in conduct, in charity, in spirit, in faith, in purity.
13 Tumia wakati wako na juhudi yako katika kusoma hadharani Maandiko Matakatifu, kuhubiri na kufundisha, mpaka nitakapokuja.
Till I come, give attendance to reading, to exhortation, to doctrine.
14 Usiache kukitumia kile kipaji cha Kristo ndani yako ulichopewa kwa maneno ya manabii na kwa kuwekewa mikono na wazee.
Neglect not the gift that is in thee, which was given thee by prophecy, with the laying on of the hands of the presbytery.
15 Fikiri kwa makini juu ya hayo yote na kuyatekeleza kusudi maendeleo yako yaonekane na wote.
Meditate upon these things; give thyself wholly to them; that thy profiting may appear to all.
16 Angalia sana mambo yako mwenyewe, na mafundisho yako. Endelea kufanya hayo maana ukifanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.
Take heed to thyself, and to thy doctrine; continue in them: for in doing this thou shalt both save thyself, and them that hear thee.