< 1 Timotheo 1 >

1 Mimi Paulo, mtume wa Yesu Kristo kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Yesu Kristo tumaini letu,
Paul, and apostle of Jesus Christ by command of God our Saviour and Jesus Christ our Hope,
2 nakuandikia Timotheo mwanangu halisi katika imani. Nakutakia neema, huruma na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Kristo Yesu Bwana wetu.
to Timothy, my true son in the faith; Grace, mercy and peace from God, our Father, and the Lord Jesus Christ.
3 Napenda ukae huko Efeso, kama nilivyokuomba nilipokuwa ninakwenda Makedonia. Wako watu fulani huko wanaofundisha mafundisho ya uongo. Wakomeshe watu hao.
As I begged you when I was setting out for Macedonia, stay where you are at Ephesus, and instruct certain individuals there not to be teaching heterodoxy,
4 Waambie waachane na zile hadithi tupu na orodha ndefu za mababu, ambazo huleta tu ubishi, wala haviwajengi watu katika mpango ujulikanao kwa imani.
nor to be paying attention to myths and interminable genealogies, which tend to promote discussions rather than a stewardship entrusted by God, a stewardship which is in faith.
5 Shabaha ya amri hii ni kuhimiza mapendo yatokayo katika moyo safi, dhamiri njema, na imani ya kweli.
Now the end of the exhortation is love, out of a pure heart and a good conscience and an undissembled faith.
6 Watu wengine wamepotoka na kugeukia majadiliano yasiyo na maana.
Some have failed here, and have turned aside to empty argument.
7 Wanapenda kuwa walimu wa Sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayosisitiza.
Although they desire to be teachers of the law, they understand neither the words they use nor the subjects they talk about.
8 Twajua kwamba Sheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo.
I know well that "the Law is good" if a man use it lawfully;
9 Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale;
but he must remember that the Law is not enacted for a good man, but for the lawless and rebellious, for the irreligious and sinful, for the godless and profane, for parricides and murderers,
10 sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba watu, waongo, na wanaoapa uongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho ya kweli.
for the immoral, for sexual perverts, for slave dealers, liars, perjurers, and whatever else is contrary to sound teaching,
11 Mafundisho hayo hupatikana katika Habari Njema ambayo mimi nimekabidhiwa niihubiri, Habari Njema ya Mungu mtukufu na mwenye heri.
as laid down in the glorious gospel of the blessed God, which has been entrusted to me.
12 Namshukuru Bwana wetu Yesu Kristo aliyenipa nguvu kwa ajili ya kazi yangu. Namshukuru kwa kuniona mimi kuwa ni mwaminifu, akaniteua nimtumikie,
And I am thankful to Christ Jesus our Lord, who has thus enabled me, that he accounted me faithful, and appointed me to his service,
13 ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya.
although I had formerly been a blasphemer and a persecutor and a doer of outrage. But I obtained mercy because I acted ignorantly in unbelief.
14 Lakini Bwana wetu alinijalia neema yake kwa wingi, akanipa imani na upendo katika kuungana na Kristo Yesu.
And the grace of our Lord overflowed with faith and love that is in Christ Jesus.
15 Usemi huu ni wa kuaminika, na tena unafaa kukubaliwa kabisa: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuwaokoa wenye dhambi. Nami ni mkosefu zaidi kuliko hao wote,
Faithful is the saying, and worthy of all acceptation, that "Jesus Christ came into the world to save sinners"! And there is no greater sinner than I!
16 lakini Mungu alinionea huruma, ili Kristo aonyeshe uvumilivu wake wote kwangu mimi, kama mfano kwa wale wote ambao baadaye watamwamini na kupokea uzima wa milele. (aiōnios g166)
Yet for this very cause I obtained mercy, so that in me, the chief of sinners, Jesus Christ might display all his boundless patience as an illustration for those who should later believe in him, and so gain life eternal. (aiōnios g166)
17 Kwake yeye aliye Mfalme wa milele na asiyekufa, yeye aliye Mungu pekee—kwake viwe heshima na utukufu milele na milele! Amina. (aiōn g165)
Now unto the King eternal, immortal, invisible, the only God, be glory and honor forever and ever. Amen! (aiōn g165)
18 Mwanangu Timotheo, nakukabidhi amri hii kufuatana na maneno ya unabii yaliyosemwa zamani juu yako. Yatumie maneno hayo yawe silaha yako katika kupigana vita vizuri,
This charge then, I am laying upon you, Timothy, my son, according to the predictions formerly made concerning you. Fight the good fight in the spirit of these predictions,
19 na ushike imani yako na dhamiri njema. Watu wengine hawakusikiliza dhamiri zao na hivyo wakaiharibu imani yao.
keeping fast hold of faith and a good conscience; which certain individuals have cast aside, and so made shipwreck of their faith.
20 Miongoni mwao ni Humenayo na Aleksanda ambao nimewakabidhi kwa Shetani, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.
Among them are Hymenaeus and Alexander, whom I have given over to Satan, so that they may be taught not to blaspheme.

< 1 Timotheo 1 >