< 1 Wathesalonike 3 >

1 Mwishowe hatukuweza kuvumilia zaidi. Basi, tuliamua kubaki kule Athene peke yetu,
Therefore when we couldn’t stand it any longer, we thought it good to be left behind at Athens alone,
2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,
and sent Timothy, our brother and God’s servant in the Good News of Christ, to establish you and to comfort you concerning your faith,
3 kusudi imani ya mtu yeyote miongoni mwenu isije ikafifia kwa sababu ya taabu hizo. Ninyi mnajua kwamba tunapaswa kupata mateso.
that no one would be moved by these afflictions. For you know that we are appointed to this task.
4 Maana, tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; na kama mjuavyo ndivyo ilivyotukia.
For most certainly, when we were with you, we told you beforehand that we are to suffer affliction, even as it happened, and you know.
5 Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu imepotea bure!
For this cause I also, when I couldn’t stand it any longer, sent that I might know your faith, for fear that by any means the tempter had tempted you, and our labor would have been in vain.
6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.
But Timothy has just now come to us from you, and brought us glad news of your faith and love, and that you have good memories of us always, longing to see us, even as we also long to see you.
7 Basi, habari za imani yenu zimetutia moyo katika taabu na mateso yetu yote,
For this cause, brothers, we were comforted over you in all our distress and affliction through your faith.
8 kwani sasa tunaishi kweli ikiwa ninyi mnasimama imara katika kuungana na Bwana.
For now we live, if you stand fast in the Lord.
9 Sasa twaweza kumshukuru Mungu wetu kwa ajili yenu. Tunamshukuru kwa furaha tuliyo nayo mbele yake kwa sababu yenu.
For what thanksgiving can we render again to God for you, for all the joy with which we rejoice for your sakes before our God,
10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.
night and day praying exceedingly that we may see your face and may perfect that which is lacking in your faith?
11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu.
Now may our God and Father himself, and our Lord Jesus Christ, direct our way to you.
12 Bwana awawezeshe ninyi kupendana na kuwapenda watu wote zaidi na zaidi, kama vile sisi tunavyowapenda ninyi.
May the Lord make you to increase and abound in love toward one another and toward all men, even as we also do toward you,
13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.
to the end he may establish your hearts blameless in holiness before our God and Father at the coming of our Lord Jesus with all his saints.

< 1 Wathesalonike 3 >