< 1 Petro 2 >

1 Basi, acheni uovu wote; uongo, unafiki, wivu na maneno ya kashfa visiweko tena.
Putting away therefore all wickedness, all deceit, hypocrisies, envies, and all evil speaking,
2 Kama vile watoto wachanga wanavyotamani maziwa, nanyi pia mnapaswa kuwa na hamu ya maziwa halisi ya kiroho, ili kwa nguvu yake mpate kukua na kukombolewa.
as newborn babies, long for the pure spiritual milk, that with it you may grow,
3 Kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mmegundua kwamba Bwana ni mwema.”
if indeed you have tasted that the Lord is gracious.
4 Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamani kubwa.
Come to him, a living stone, rejected indeed by men, but chosen by God, precious.
5 Mwendeeni yeye kama mawe hai mkajengeke na kuwa nyumba ya kiroho, ambamo mtatumikia kama makuhani watakatifu, kutolea dhabihu za kiroho zenye kumpendeza Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.
You also as living stones are built up as a spiritual house, to be a holy priesthood, to offer up spiritual sacrifices, acceptable to God through Jesus Christ.
6 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka huko sioni jiwe kuu la msingi, jiwe la thamani kubwa nililoliteua. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa.”
Because it is contained in Scripture, “Behold, I lay in Zion a chief cornerstone, chosen and precious. He who believes in him will not be disappointed.”
7 Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
For you who believe therefore is the honour, but for those who are disobedient, “The stone which the builders rejected has become the chief cornerstone,”
8 Tena Maandiko yasema: “Jiwe hilo ni jiwe la kujikwaa, mwamba wa kuwaangusha watu.” Watu hujikwaa kwa sababu hawauamini ule ujumbe; na ndivyo walivyopangiwa tangu mwanzo.
and, “a stumbling stone and a rock of offence.” For they stumble at the word, being disobedient, to which also they were appointed.
9 Lakini ninyi ni ukoo mteule, makuhani wa Mfalme, taifa takatifu; watu wake Mungu mwenyewe, mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyewaiteni kutoka gizani akawaingizeni katika mwanga wake mkuu.
But you are a chosen race, a royal priesthood, a holy nation, a people for God’s own possession, that you may proclaim the excellence of him who called you out of darkness into his marvellous light.
10 Wakati mmoja ninyi hamkuwa watu wa Mungu, lakini sasa ninyi ni watu wake; wakati mmoja hamkupewa huruma ya Mungu, lakini sasa mmeipokea.
In the past, you were not a people, but now are God’s people, who had not obtained mercy, but now have obtained mercy.
11 Wapenzi wangu, nawasihi ninyi kama wageni na wakimbizi hapa duniani! Achaneni na tamaa za mwili ambazo hupingana na roho.
Beloved, I beg you as foreigners and pilgrims to abstain from fleshly lusts which war against the soul,
12 Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu Siku ya kuja kwake.
having good behaviour amongst the nations, so in that of which they speak against you as evildoers, they may see your good works and glorify God in the day of visitation.
13 Basi, jiwekeni chini ya mamlaka yote ya kibinadamu, kwa ajili ya Bwana: utii kwa mfalme aliye mtawala mkuu,
Therefore subject yourselves to every ordinance of man for the Lord’s sake: whether to the king, as supreme,
14 utii kwa wakuu wa mikoa ambao wameteuliwa naye kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema.
or to governors, as sent by him for vengeance on evildoers and for praise to those who do well.
15 Maana Mungu anataka mweze kuyakomesha maneno ya kijinga ya watu wasio na akili kwa matendo mema mnayofanya.
For this is the will of God, that by well-doing you should put to silence the ignorance of foolish men.
16 Ishini kama watu huru; lakini msiutumie uhuru wenu kuuficha ubaya, bali ishini kama watumishi wa Mungu.
Live as free people, yet not using your freedom for a cloak of wickedness, but as bondservants of God.
17 Waheshimuni watu wote, wapendeni ndugu zenu waumini, mcheni Mungu, mheshimuni mfalme.
Honour all men. Love the brotherhood. Fear God. Honour the king.
18 Enyi watumishi wa nyumbani, watiini wakuu wenu kwa heshima yote, wawe wema na wapole au wenye kuchukiza.
Servants, be in subjection to your masters with all respect, not only to the good and gentle, but also to the wicked.
19 Maana kama mnavumilia maumivu ya mateso msiyostahili kwa sababu mwajua kwamba Mungu anataka hivyo, basi Mungu atawafadhili.
For it is commendable if someone endures pain, suffering unjustly, because of conscience towards God.
20 Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
For what glory is it if, when you sin, you patiently endure beating? But if when you do well, you patiently endure suffering, this is commendable with God.
21 Hayo ndiyo mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ili muufuate mwenendo wake.
For you were called to this, because Christ also suffered for us, leaving you an example, that you should follow his steps,
22 Yeye hakutenda dhambi, wala neno la udanganyifu halikusikika mdomoni mwake.
who didn’t sin, “neither was deceit found in his mouth.”
23 Alipotukanwa yeye hakujibu kwa tukano; alipoteseka yeye hakutoa vitisho, bali aliyaweka matumaini yake kwa Mungu, hakimu mwenye haki.
When he was cursed, he didn’t curse back. When he suffered, he didn’t threaten, but committed himself to him who judges righteously.
24 Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake juu ya msalaba, tupate kufa kuhusu dhambi, na kuishi kwa ajili ya uadilifu. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.
He himself bore our sins in his body on the tree, that we, having died to sins, might live to righteousness. You were healed by his wounds.
25 Ninyi mlikuwa kama kondoo waliokuwa wamepotea; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
For you were going astray like sheep; but now you have returned to the Shepherd and Overseer of your souls.

< 1 Petro 2 >