< 1 Petro 1 >

1 Mimi Petro, mtume wa Yesu Kristo nawaandikia ninyi wateule wa Mungu Baba, ambao mmetawanyika na mnaishi kama wakimbizi huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithunia.
Peter, an apostle of Jesus Christ, To the elect who are exiles of the Dispersion throughout Pontus, Galatia, Cappadocia, Asia, and Bithynia, chosen
2 Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
according to the foreknowledge of God the Father and sanctified by the Spirit for obedience to Jesus Christ and sprinkling by His blood: Grace and peace be yours in abundance.
3 Asifiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa huruma yake kuu alitufanya tuzaliwe upya kwa kumfufua Yesu kutoka wafu. Ametujalia tumaini lenye uzima,
Blessed be the God and Father of our Lord Jesus Christ! By His great mercy He has given us new birth into a living hope through the resurrection of Jesus Christ from the dead,
4 na hivyo tunatazamia kupata baraka zile ambazo Mungu aliwawekea watu wake. Mungu amewawekeeni baraka hizo mbinguni ambako haziwezi kuoza au kuharibika au kufifia.
and into an inheritance that is imperishable, undefiled, and unfading, reserved in heaven for you,
5 Hizo zitakuwa zenu ninyi ambao kwa imani mnalindwa salama kwa nguvu ya Mungu kwa ajili ya wokovu ambao uko tayari kufunuliwa mwishoni mwa nyakati.
who through faith are shielded by God’s power for the salvation that is ready to be revealed in the last time.
6 Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.
In this you greatly rejoice, though now for a little while you may have had to suffer grief in various trials
7 Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
so that the proven character of your faith—more precious than gold, which perishes even though refined by fire—may result in praise, glory, and honor at the revelation of Jesus Christ.
8 Ninyi mnampenda ingawaje hamjamwona, na mnamwamini ingawa hamumwoni sasa. Hivyo, mnafurahi kwa furaha tukufu isiyoelezeka,
Though you have not seen Him, you love Him; and though you do not see Him now, you believe in Him and rejoice with an inexpressible and glorious joy,
9 kwa sababu mnapokea wokovu wa roho zenu ambao ni lengo la imani yenu.
now that you are receiving the goal of your faith, the salvation of your souls.
10 Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.
Concerning this salvation, the prophets who foretold the grace to come to you searched and investigated carefully,
11 Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
trying to determine the time and setting to which the Spirit of Christ in them was pointing when He predicted the sufferings of Christ and the glories to follow.
12 Mungu aliwafunulia kwamba wakati walipokuwa wanasema juu ya hayo mambo ambayo ninyi mmekwisha sikia sasa kutoka kwa wale wajumbe waliowatangazieni Habari Njema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, hiyo kazi yao haikuwa kwa faida yao wenyewe, bali kwa ajili yenu. Hayo ndiyo mambo ambayo hata malaika wangependa kuyafahamu.
It was revealed to them that they were not serving themselves, but you, when they foretold the things now announced by those who preached the gospel to you by the Holy Spirit sent from heaven. Even angels long to look into these things.
13 Kwa hiyo, basi, muwe tayari kabisa kwa nia, na kukesha. Wekeni tumaini lenu lote katika baraka ile mtakayopewa wakati Yesu Kristo atakapoonekana!
Therefore prepare your minds for action. Be sober-minded. Set your hope fully on the grace to be given you at the revelation of Jesus Christ.
14 Kama watoto wa Mungu wenye utii, msikubali kamwe kufuata tena tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mlipokuwa wajinga.
As obedient children, do not conform to the passions of your former ignorance.
15 Bali mnapaswa kuwa watakatifu katika mwenendo wenu wote, kama vile yule aliyewaiteni ni mtakatifu.
But just as He who called you is holy, so be holy in all you do,
16 Maandiko yasema: “Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”
for it is written: “Be holy, because I am holy.”
17 Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
Since you call on a Father who judges each one’s work impartially, conduct yourselves in reverent fear during your stay as foreigners.
18 Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
For you know that it was not with perishable things such as silver or gold that you were redeemed from the empty way of life you inherited from your forefathers,
19 bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
but with the precious blood of Christ, a lamb without blemish or spot.
20 Yeye alikuwa ameteuliwa na Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa, akafunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu.
He was known before the foundation of the world, but was revealed in the last times for your sake.
21 Kwa njia yake, ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka wafu na kumpa utukufu; na hivyo imani na matumaini yenu yako kwa Mungu.
Through Him you believe in God, who raised Him from the dead and glorified Him; and so your faith and hope are in God.
22 Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
Since you have purified your souls by obedience to the truth so that you have a genuine love for your brothers, love one another deeply, from a pure heart.
23 Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele. (aiōn g165)
For you have been born again, not of perishable seed, but of imperishable, through the living and enduring word of God. (aiōn g165)
24 Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama nyasi, na utukufu wake wote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyauka na maua huanguka.
For, “All flesh is like grass, and all its glory like the flowers of the field; the grass withers and the flowers fall,
25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.” Neno hilo ni hiyo Habari Njema iliyohubiriwa kwenu. (aiōn g165)
but the word of the Lord stands forever.” And this is the word that was proclaimed to you. (aiōn g165)

< 1 Petro 1 >