< 1 Wakorintho 1 >

1 Mimi Paulo, niliyeitwa kuwa mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Sosthene,
Paul, a called apostle of Christ Jesus, through the will of God, and Sosthenes the brother,
2 tunawaandikia ninyi mlio kanisa la Mungu huko Korintho. Ninyi mmefanywa watakatifu katika kuungana na Kristo Yesu, mkaitwa muwe watu wa Mungu, pamoja na watu wote popote wanaomwomba Bwana wetu Yesu Kristo aliye Bwana wao na wetu pia.
to the church of God which is at Corinth, the sanctified in Christ Jesus, called, holy, with all that in every place call upon the name of our Lord Jesus Christ, their Lord and ours;
3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
grace be to you, and peace, from God our Father, and the Lord Jesus Christ.
4 Ninamshukuru Mungu wangu daima kwa ajili yenu kwa sababu amewatunukia ninyi neema yake kwa njia ya Kristo Yesu.
I ever thank my God for you, on account of the grace of God bestowed upon you in Christ Jesus;
5 Maana, kwa kuungana na Kristo mmetajirishwa katika kila kitu. Mmejaliwa elimu yote na uwezo wote wa kuhubiri,
that in him ye were enriched in everything, in all utterance, and all knowledge,
6 kwani, ujumbe juu ya Kristo umethibitishwa ndani yenu,
as the testimony of Christ was established among you;
7 hata hampungukiwi kipaji chochote cha kiroho mkiwa mnangojea kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
so that ye come behind in no gift, while waiting for the manifestation of our Lord Jesus Christ;
8 Yeye atawaimarisha ninyi mpaka mwisho mpate kuonekana bila hatia Siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
who will also make you steadfast to the end, so that ye may be without blame in the day of our Lord Jesus Christ.
9 Mungu ni mwaminifu; yeye aliwaita ninyi muwe na umoja na Mwanae Yesu Kristo Bwana wetu.
God is faithful, by whom ye were called into the fellowship of his Son Jesus Christ our Lord.
10 Ndugu, ninawasihi kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo: pataneni nyote katika kila jambo msemalo; yasiweko mafarakano kati yenu; muwe na fikira moja na nia moja.
But I beseech you, brethren, by the name of our Lord Jesus Christ, that ye all speak the same thing, and that there be no divisions among you, but that ye be perfectly united in the same mind and in the same judgment.
11 Ndugu zangu, habari nilizopata kutoka kwa watu kadhaa wa jamaa ya Kloe, zaonyesha wazi kwamba kuna kutoelewana kati yenu.
For I have been informed concerning you, my brethren, by those of the family of Chloe, that there are dissensions among you.
12 Nataka kusema hivi: kila mmoja anasema chake: mmoja husema, “Mimi ni wa Paulo,” mwingine: “Mimi ni wa Apolo,” mwingine: “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine: “Mimi ni wa Kristo,”.
What I mean is this, that each of you saith, I am of Paul; and I of Apollos; and I of Cephas; and I of Christ.
13 Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye aliyesulubiwa kwa ajili yenu? Au je, mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Is Christ divided? Was Paul crucified for you? Or were ye baptized the name of Paul?
14 Namshukuru Mungu kwamba sikumbatiza mtu yeyote miongoni mwenu isipokuwa tu Krispo na Gayo.
I thank God that I baptized none of you, but Crispus and Gaius;
15 Kwa hiyo hakuna awezaye kusema amebatizwa kwa jina langu.
that no one may say that ye were baptized into my name.
16 (Samahani, nilibatiza pia jamaa ya Stefana; lakini zaidi ya hawa, sidhani kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.)
And I baptized also the household of Stephanas; I am not aware that I baptized any one besides.
17 Kristo hakunituma kubatiza, bali kuhubiri Habari Njema; tena, niihubiri bila kutegemea maarifa ya hotuba za watu kusudi nguvu ya kifo cha Kristo msalabani isibatilishwe.
For Christ sent me not to baptize, but to preach the gospel; not with wisdom of speech, lest the cross of Christ should be made of no effect.
18 Maana ujumbe kuhusu kifo cha Kristo msalabani ni jambo la kipumbavu kwa wale walio katika mkumbo wa kupotea, lakini kwetu sisi tulio katika njia ya wokovu ujumbe huo ni nguvu ya Mungu.
For the preaching of the cross is to those who are perishing, foolishness, but to us who are being saved, it is the power of God.
19 Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na elimu ya wataalamu nitaitupilia mbali.”
For it is written: “I will destroy the wisdom of the wise, and will bring to nought the discernment of the discerning.”
20 Yu wapi basi, mwenye hekima? Yu wapi basi, mwalimu wa Sheria? Naye bingwa wa mabishano wa nyakati hizi yuko wapi? Mungu ameifanya hekima ya ulimwengu kuwa upumbavu. (aiōn g165)
Where is the wise man? Where the scribe? Where the disputer of this world? Hath not God made foolish the wisdom of the world? (aiōn g165)
21 Maana, kadiri ya hekima ya Mungu, watu hawawezi kumjua Mungu kwa njia ya hekima yao wenyewe. Badala yake, Mungu amependa kuwaokoa wale wanaoamini kwa njia ya kile ambacho wenye hekima wanakiona kuwa ni upumbavu, yaani ujumbe tunaohubiri.
For since, in the wisdom of God, the world by its wisdom knew not God, it pleased God by the foolishness of preaching to save those who believe;
22 Wayahudi wanataka ishara, na Wagiriki wanatafuta hekima;
since even Jews ask for signs, and the Greeks seek for wisdom;
23 lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa. Kwa Wayahudi jambo hili ni kikwazo, na kwa watu wa mataifa ni upumbavu;
but we preach Christ crucified, to Jews a stumbling-block, and to gentiles foolishness,
24 lakini kwa wale walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu.
but to those who are called, both Jews and Greeks, Christ the power of God, and the wisdom of God.
25 Maana kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko nguvu za binadamu.
Because the foolishness of God is wiser than men; and the weakness of God is stronger than men.
26 Ndugu, kumbukeni wakati mlipoitwa: wengi wenu hawakuwa wenye hekima hata kwa fikira za binadamu; wengi hawakuwa wenye nguvu au watu wa tabaka ya juu.
For consider, brethren, who ye are that have been called; not many wise men after the fashion of the world, not many mighty, not many noble;
27 Ndiyo kusema, Mungu aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni upumbavu, ili awaaibishe wenye hekima; na aliyachagua yale ambayo ulimwengu huyaona ni dhaifu, ili awaaibishe wenye nguvu.
but the foolish things of the world did God choose, to put to shame the wise; and the weak things of the world did God choose, to put to shame the things which are strong;
28 Mungu ameyachagua yale ambayo kwa fikira za dunia ni mambo yaliyo duni na yanayodharauliwa, mambo ambayo hata hayakuwako, ili kwa hayo ayafutilie mbali yale ambayo kwa fikira za binadamu ni mambo ya maana.
and the mean things of the world, and the things which are despised, did God choose, the things which are not, to bring to nought things that are;
29 Basi, hakuna mtu awezaye kujivunia chochote mbele ya Mungu.
that no flesh might glory before God.
30 Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha ninyi na Kristo Yesu. Mungu amemfanya Kristo awe hekima yetu; kwa njia yake sisi tunapatanishwa na Mungu, tunakuwa watu wake Mungu na kukombolewa.
But from him it is that ye are in Christ Jesus, who from God was made to us wisdom, and righteousness, and sanctification, and redemption;
31 Basi, kama yasemavyo Maandiko Matakatifu: “Mwenye kutaka kujivuna, basi, na ajivunie kazi ya Bwana.”
that, according as it is written, “He that glorieth, let him glory in the Lord.”

< 1 Wakorintho 1 >