< 1 Wakorintho 9 >

1 Je, mimi si mtu huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Je, ninyi si matokeo ya kazi yangu kwa ajili ya Bwana?
Am I not free? Am I not an apostle? Have I not seen Jesus our Lord? Are you not my work in the Lord?
2 Hata kama kwa watu wengine mimi si mtume, lakini walau kwenu ninyi mimi ni mtume. Ninyi ni uthibitisho wa mtume wangu kwa sababu ya kuungana kwenu na Bwana.
Even if I am not an apostle to others, to you at least I am; for you are the seal of my apostleship in the Lord.
3 Hoja yangu kwa wale wanaonipinga ndiyo hii:
This is my reply to my critics.
4 Je, hatuna haki ya kula na kunywa?
Have I no right to claim food and drink?
5 Je, hatuna ruhusa kumchukua mke Mkristo katika ziara zetu, kama vile wafanyavyo mitume wengine, ndugu zake Bwana, na pia Kefa?
Have I no right to take a believing wife with me on my journey, as the rest of the apostles and the Lord’s brothers and Peter do?
6 Au ni mimi tu na Barnaba ambao tunapaswa kujipatia maslahi yetu kwa kufanya kazi?
Are we the only ones, Barnabas and I, who have no right to give up manual labor?
7 Je, mwanajeshi gani anayelipia utumishi wake jeshini? Mkulima gani asiyekula matunda ya shamba lake la mizabibu? Mchungaji gani asiyekunywa maziwa ya mifugo yake?
What soldier ever serves at his own expense? What farmer ever plants a vineyard and his flock and does not taste the milk?
8 Je, nasema mambo haya kibinadamu tu? Je, Sheria nayo haisemi hivyo?
Am I saying this on human authority only, or does not the Law also say the same?
9 Imeandikwa katika Sheria ya Mose: “Usimfunge kinywa ng'ombe anapoliwata nafaka.” Je, ndio kusema Mungu anajishughulisha na ng'ombe?
Yea, in the Law of Moses it is written, Thou shalt not muzzle an ox while he is treading out the grain.
10 Je, hakuwa anatufikiria sisi aliposema hivyo? Naam, haya yaliandikwa kwa ajili yetu; kwani yule anayelima na yule anayevuna, wote wawili wana haki ya kutumaini kupata sehemu ya mavuno.
Is it the oxen that God is thinking about, or is it really said for our sakes? It was written for us; because the plowman ought to plow in hope, and the thresher in hope of getting a share of the crop.
11 Ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, je, ni jambo kubwa tukichuma kwenu faida ya kidunia?
If I have sown for you the seeds of spiritual good, is it a great thing if I reap from you temporal goods?
12 Ikiwa wengine wanayo haki ya kutazamia hayo kutoka kwenu, je, sisi hatuna haki zaidi kuliko hao? Lakini, sisi hatukuitumia haki hiyo, Badala yake, tumestahimili kila kitu ili tusiiwekee kizuizi chochote Habari Njema ya Kristo.
If others share this authority over you, do not I far more? Yet I have not availed myself of it, but am patiently enduring; so that I may not in any way hinder the progress of Christ’s gospel.
13 Je, hamjui kwamba wanaotumikia Hekaluni hupata chakula chao Hekaluni, na kwamba wanaotolea sadaka madhabahuni hupata sehemu ya hiyo sadaka?
You know, do you not, that those who minister in the temple, and those who serve at the altar, get their portion of the sacrifices?
14 Bwana aliagiza vivyo hivyo; wahubiri wa Habari Njema wapate riziki zao kutokana nayo.
Even so the Lord ordained that those who proclaim the gospel should get their living by the gospel.
15 Lakini, mimi sikutumia hata mojawapo ya haki hizo. Na wala siandiki nijipatie haki hizo; kwangu mimi ni afadhali kufa kuliko kumfanya yeyote aone kwamba najisifu bure.
But for my part, I have never availed myself of any of these rights. I do not say this to bring it about in my own case. I would rather die than let any one make void this boast of mine.
16 Ikiwa ninaihubiri Habari Njema, hilo si jambo la kujivunia; hilo ni jukumu nililopewa. Na, ole wangu kama sitaihubiri Habari Njema!
Proclaiming the gospel gives me no ground of boasting; for necessity is laid upon me; woe is me if I preach not the gospel.
17 Ningekuwa nimeichagua kazi hii kwa hiari, basi, ningetazamia malipo; lakini maadam naifanya ikiwa ni wajibu, hiyo ina maana kwamba ni jukumu nililopewa nitekeleze.
For if I do this of my own accord, I have my pay; but if unwilling, I have at least discharged my stewardship.
18 Mshahara wangu ni kitu gani, basi? Mshahara wangu ni fursa ya kuihubiri Habari Njema bure, bila kudai haki ninazostahili kwa kuihubiri.
What then is my wage? This, that I can make the gospel free where I carry it; and that I can refrain from using my rights as a preacher of the gospel.
19 Kwa hiyo, ingawa mimi si mtumwa wa mtu yeyote, nimejifanya mtumwa wa kila mtu ili nimpatie Kristo watu wengi iwezekanavyo.
Though free from all men, I make myself the slave of all, that I may win the more.
20 Kwa Wayahudi nimeishi kama Myahudi ili niwapate Wayahudi; yaani, ingawa mimi siko chini ya Sheria, nimejiweka chini ya Sheria kwao, ili niwapate hao walio chini ya Sheria.
To the Jews I am become like a Jew, that I may win Jews; to those under the Law, like one under the Law, though I am not under the Law, myself;
21 Na kwa wale walio nje ya Sheria, naishi kama wao, nje ya Sheria, ili niwapate hao walio nje ya Sheria. Hii haimaanishi kwamba mimi niko nje ya sheria ya Mungu, maana nabanwa na sheria ya Kristo.
to those outside the Law, as one outside the Law, to win those outside the Law (though I am not outside the law of God, but inside the law of Christ).
22 Kwao walio dhaifu nimejifanya dhaifu ili niwapate hao walio dhaifu. Nimejifanya kila kitu kwa wote ili nipate kuwaokoa baadhi yao kwa kila njia.
I am become weak to the weak, to win the weak. I am become all these things to all men that, by any and by all means, I may save some.
23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Habari Njema, nipate kushiriki baraka zake.
And I am doing it all for the gospel’s sake, that I may become a copartner in it.
24 Je, hamjui kwamba katika uwanja wa michezo, ingawa wapiga mbio wote hukimbia, ni mmoja tu anayejinyakulia zawadi?
Do you not know that in a foot-race, though all run, only one receives the prize? So run that you may win.
25 Wanariadha hujipa mazoezi na nidhamu kali; hufanya hivyo ili wajipatie taji iharibikayo! Lakini sisi twafanya hivyo tupate taji ya kudumu daima.
Every man who contends in the games continually trains himself by all manner of self-restraint. Now they do it to get a fading garland, but we, one that is unfading.
26 Ndivyo basi, ninavyopiga mbio nikiwa na nia ya kushinda; ndivyo ninavyopigana, na si kama bondia anayetupa ngumi zake hewani.
For my part, then, I run with no wavering to the goal. I box not as one beating the air,
27 Naupa mwili wangu mazoezi magumu na kuutia katika nidhamu kamili, nisije mimi mwenyewe nikakataliwa baada ya kuwahubiria wengine.
but I bruise my body and keep it in subjection, lest having called others to the contest, I should myself be disqualified.

< 1 Wakorintho 9 >