< 1 Wakorintho 8 >
1 Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga.
Now concerning things sacrificed to idols: We know that we all have knowledge. Knowledge puffs up, but love builds up.
2 Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
But if anyone thinks that he knows anything, he does not yet know as he ought to know.
3 Lakini anayempenda Mungu huyo anajulikana naye.
But if anyone loves God, this one is known by him.
4 Kwa hiyo, kuhusu vyakula vilivyotambikiwa sanamu, twajua kwamba sanamu si kitu duniani; twajua kwamba Mungu ni mmoja tu.
Therefore concerning the eating of things sacrificed to idols, we know that no idol is anything in the world, and that there is no God but one.
5 Hata kama viko vitu viitwavyo miungu duniani au mbinguni, na hata kama wako miungu na mabwana wengi,
For though there are things that are called "gods," whether in the heavens or on earth; as there are many "gods" and many "lords;"
6 hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu: Baba, Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko. Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo, ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa, na sisi twaishi kwa njia yake.
yet to us there is one God, the Father, from whom are all things, and we for him; and one Lord, Yeshua Meshikha, through whom are all things, and we live through him.
7 Lakini, si kila mtu anao ujuzi huu. Maana wako watu wengine waliokwisha zoea sanamu, watu ambao mpaka hivi sasa wanapokula vyakula huviona bado kama vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Na kwa vile dhamiri zao ni dhaifu, hutiwa unajisi.
However, not all have this knowledge. But some, being so accustomed to idols until now, eat as of a thing sacrificed to an idol, and their conscience, being weak, is defiled.
8 Lakini chakula hakiwezi kutupeleka karibu zaidi na Mungu. Tukiacha kukila hatupungukiwi kitu, tukikila hatuongezewi kitu.
But food will not commend us to God. For neither, if we do not eat, are we the worse; nor, if we eat, are we the better.
9 Lakini, jihadharini: huu uhuru wenu usiwafanye walio na imani dhaifu waanguke katika dhambi.
But be careful that by no means does this liberty of yours become a stumbling block to the weak.
10 Maana, mtu ambaye dhamiri yake ni dhaifu, akikuona wewe mwenye ujuzi unakula vyakula hivyo ndani ya hekalu la sanamu, je, hatatiwa moyo wa kula vyakula vilivyotambikiwa sanamu?
For if someone sees you who have knowledge sitting in an idol's temple, won't his conscience, if he is weak, be emboldened to eat things sacrificed to idols?
11 Hivyo, huyo ndugu yako dhaifu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake, atapotea kwa sababu ya ujuzi wako.
And through your knowledge, he who is weak perishes, the brother for whom the Meshikha died.
12 Kama mkiwakosesha ndugu zenu jinsi hiyo na kuzijeruhi dhamiri zao dhaifu, mtakuwa mmemkosea Kristo.
Thus, sinning against the brothers, and wounding their conscience when it is weak, you sin against Meshikha.
13 Kwa hiyo, ikiwa chakula husababisha kuanguka kwa ndugu yangu, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi. (aiōn )
Therefore, if food causes my brother to stumble, I will eat no meat forevermore, that I do not cause my brother to stumble. (aiōn )