< 1 Wakorintho 15 >
1 Sasa ndugu, napenda kuwakumbusha ile Habari Njema niliyowahubirieni nanyi mkaipokea na kusimama imara ndani yake.
Now I declare to you, brothers, the Good News which I preached to you, which also you received, in which you also stand,
2 Kwa njia yake mnaokolewa, ikiwa mnayazingatia maneno niliyowahubirieni, na kama kuamini kwenu hakukuwa bure.
by which also you are saved, if you hold firmly the word which I preached to you—unless you believed in vain.
3 Mimi niliwakabidhi ninyi mambo muhimu sana ambayo mimi niliyapokea: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kufuatana na Maandiko Matakatifu;
For I delivered to you first of all that which I also received: that Christ died for our sins according to the Scriptures,
4 kwamba alizikwa, akafufuka siku ya tatu kama ilivyoandikwa;
that he was buried, that he was raised on the third day according to the Scriptures,
5 kwamba alimtokea Kefa, na baadaye aliwatokea wale kumi na wawili.
and that he appeared to Cephas, then to the twelve.
6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
After that he appeared to over five hundred brothers at once, most of whom remain until now, but some have also fallen asleep.
7 Baadaye alimtokea Yakobo kisha akawatokea mitume wote.
After that he appeared to James, then to all the apostles,
8 Baada ya wote, akanitokea hata mimi, mimi niliyekuwa kama mtu aliyezaliwa kabla ya wakati.
and last of all, as to the child born at the wrong time, he appeared to me also.
9 Maana mimi ni mdogo kabisa miongoni mwa mitume na wala sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililidhulumu kanisa la Mungu.
For I am the least of the apostles, who is not worthy to be called an apostle, because I persecuted the church of God.
10 Lakini, kwa neema yake Mungu, nimekuwa kama nilivyo. Na neema yake kwangu haikuwa bure. Mimi nimefanya kazi kuliko wote; si mimi hasa, ila ni neema ya Mungu ifanyayo kazi pamoja nami.
But by the grace of God I am what I am. His grace which was bestowed on me was not futile, but I worked more than all of them; yet not I, but the grace of God which was with me.
11 Lakini hata hivyo, iwe wao ndio wahubirio au mimi nihubiriye, haidhuru, hiki ndicho tunachuhubiri, na hiki ndicho mnachoamini.
Whether then it was I or they, this is what we preach, and this is what you believed.
12 Sasa, maadam inahubiriwa kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, baadhi yenu wanawezaje kusema kwamba hakuna ufufuo wa wafu?
Now if Christ is preached, that he has been raised from the dead, how do some among you say that there is no resurrection of the dead?
13 Kama hakuna ufufuo wa wafu, basi, Kristo naye hakufufuka;
But if there is no resurrection of the dead, neither has Christ been raised.
14 na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yenu haina maana.
If Christ has not been raised, then our preaching is in vain, and your faith also is in vain.
15 Zaidi ya hayo sisi tungekuwa mashahidi wa uongo mbele ya Mungu, maana tulisema kwamba Mungu alimfufua Kristo kutoka wafu na kumbe yeye hakumfufua—kama ni kweli kwamba wafu hawafufuliwi.
Yes, we are found false witnesses of God, because we testified about God that he raised up Christ, whom he did not raise up, if it is so that the dead are not raised.
16 Maana, ikiwa ni kweli kwamba wafu hawafufuki, basi naye Kristo hakufufuka.
For if the dead are not raised, neither has Christ been raised.
17 Na kama Kristo hakufufuliwa, basi, imani yenu ni ya bure; mngali bado katika dhambi zenu.
If Christ has not been raised, your faith is vain; you are still in your sins.
18 Zaidi ya hayo, wale wote waliokufa wakiwa wameungana na Kristo wamepotea kabisa.
Then they also who are fallen asleep in Christ have perished.
19 Kama matumaini yetu katika Kristo yanahusu tu maisha haya ya sasa, basi, sisi ni watu wa kusikitikiwa zaidi kuliko wengine wote duniani.
If we have only hoped in Christ in this life, we are of all people most to be pitied.
20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka wafu, limbuko lao wale waliolala katika kifo.
But now Christ has been raised from the dead, the first fruits of those who are asleep.
21 Maana kama vile kifo kilivyoletwa duniani na mtu mmoja, vivyo hivyo nako kufufuka kutoka wafu kumesababishwa na mtu mmoja.
For since death came by man, the resurrection of the dead also came by man.
22 Kama vile watu wote wanavyokufa kwa kujiunga na Adamu, vivyo hivyo wote watafufuliwa kwa kuungana na Kristo.
For as in Adam all die, so also in Christ all will be made alive.
23 Lakini kila mmoja kwa mpango wake: Kristo kwanza, halafu wale walio wake Kristo wakati Kristo atakapokuja.
But each in his own order: Christ the first fruits, then those who are Christ's, at his coming.
24 Baada ya hayo, mwisho utafika wakati ambapo Kristo atamkabidhi Mungu Baba Utawala, baada ya kufutilia mbali kila tawala na mamlaka na nguvu.
Then the end comes, when he will deliver up the Kingdom to God, even the Father; when he will have abolished all rule and all authority and power.
25 Maana Kristo sharti atawale mpaka Mungu atakapowashinda adui zake na kuwaweka chini ya miguu yake.
For he must reign until he has put all his enemies under his feet.
26 Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni kifo.
The last enemy that will be abolished is death.
27 Maana, Maandiko yasema: “Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini, Maandiko yanaposema: “Vitu vyote vimewekwa chini ya miguu yake avitawale” ni dhahiri kwamba Mungu haingii katika kundi hilo la vitu, maana yeye ndiye anayeviweka vitu hivyo chini ya Kristo.
For, "He put all things under his feet." But when he says "all things" are put under, it is evident that the one who put all things under is the exception.
28 Lakini vitu vyote vitakapowekwa chini ya Utawala wa Kristo, ndipo naye Mwana atakapojiweka chini ya Mungu, aliyeweka vyote chini ya Utawala wake; ili Mungu atawale juu ya vyote.
When all things have been subjected to him, then the Son will also himself be subjected to him who subjected all things to him, that God may be all in all.
29 Kama hakuna ufufuo, je watu wale wanaobatizwa kwa ajili ya wafu wanatumainia kupata nini? Kama wafu hawafufuliwi, ya nini kubatizwa kwa ajili yao?
Or else what will they do who are baptized for the dead? If the dead are not raised at all, why then are they baptized for them?
30 Na sisi, ya nini kujitia hatarini kila saa?
Why do we also stand in jeopardy every hour?
31 Ndugu, mimi nakikabili kifo kila siku! Fahari niliyo nayo juu yenu katika kuungana na Kristo Yesu Bwana wetu inanifanya nitangaze jambo hili.
I affirm, brothers, by the boasting in you which I have in Christ Jesus our Lord, I die daily.
32 Kama kusudi langu lingalikuwa la kibinadamu tu, kule kupigana kwangu na wanyama wakali hapa Efeso kungalinifaa kitu gani? Kama wafu hawafufuki, basi, “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa.”
If I fought with animals at Ephesus for human purposes, what does it profit me? If the dead are not raised, then "let us eat and drink, for tomorrow we die."
33 Msidanganyike! Urafiki mbaya huharibu tabia njema.
Do not be deceived. "Bad company corrupts good morals."
34 Amkeni! Anzeni kuishi vema, na acheni kutenda dhambi. Baadhi yenu hawamjui Mungu kabisa. Hii nawaambieni, ni aibu kubwa kwenu!
Become sober-minded, and do not sin, for some are ignorant about God. I say this to your shame.
35 Lakini mtu anaweza kuuliza: “Wafu watafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani wakati watakapokuja tena?”
But someone will say, "How are the dead raised?" and, "With what kind of body do they come?"
36 Hayo ni maswali ya kijinga! Ukipanda mbegu, isipokufa kwanza haitaota.
You foolish one, that which you yourself sow is not made alive unless it dies.
37 Unachopanda ni mbegu tu, labda ya ngano au nafaka nyingine, na si mmea mzima ambao hutokea baadaye.
That which you sow, you do not sow the body that will be, but a bare grain, maybe of wheat, or of some other kind.
38 Mungu huipa hiyo mbegu mwili anaoutaka mwenyewe; kila mbegu hupata mwili wake wa pekee.
But God gives it a body even as it pleased him, and to each seed a body of its own.
39 Miili ya viumbe vyote si sawa. Miili ya binadamu ni ya namna moja, ya wanyama ni ya namna nyingine, ya ndege ni ya namna nyingine na miili ya samaki pia ni ya namna nyingine.
All flesh is not the same flesh, but there is one flesh of humans, another flesh of animals, another of fish, and another of birds.
40 Iko miili ya mbinguni na miili ya duniani; uzuri wa miili ya mbinguni ni mwingine, na na uzuri wa miili ya duniani ni mwingine.
There are also celestial bodies, and terrestrial bodies; but the glory of the celestial differs from that of the terrestrial.
41 Uko uzuri wa jua, wa mwezi na wa nyota; hata nyota nazo huhitilafiana kwa uzuri.
There is one glory of the sun, another glory of the moon, and another glory of the stars; for one star differs from another star in glory.
42 Ndivyo ilivyo kuhusu ufufuo wa wafu. Kama vile mbegu, mwili huzikwa ardhini ukiwa katika hali ya kuharibika, lakini hufufuliwa katika hali ya kutoharibika.
So also is the resurrection of the dead. It is sown in corruption; it is raised in incorruption.
43 Huzikwa katika hali duni, hufufuliwa katika hali tukufu; huzikwa katika hali dhaifu, hufufuliwa ukiwa wenye nguvu.
It is sown in dishonor; it is raised in glory. It is sown in weakness; it is raised in power.
44 Unapozikwa ni mwili wa kawaida, unapofufuliwa ni mwili wa kiroho. Kuna mwili wa kawaida na kutakuwa na mwili wa kiroho.
It is sown a natural body; it is raised a spiritual body. There is a natural body and there is also a spiritual body.
45 Maana Maandiko yasema: “Mtu wa kwanza, Adamu, alikuwa kiumbe mwenye uhai;” lakini adamu wa mwisho ni Roho awapaye watu uzima.
So also it is written, "The first man, Adam, became a living soul." The last Adam became a life-giving spirit.
46 Lakini unaotangulia kuwako si ule mwili wa kiroho, ila ule mwili wa kawaida kisha ule mwili wa kiroho.
However that which is spiritual is not first, but that which is natural, then that which is spiritual.
47 Adamu wa kwanza aliumbwa kwa udongo, alitoka ardhini; mtu wa pili alitoka mbinguni.
The first man is of the earth, made of dust. The second man is from heaven.
48 Wote walio wa dunia wako kama huyo mtu aliyeumbwa kwa udongo; wale walio wa mbinguni wako kama yule aliyetoka mbinguni.
As is the one made of dust, such are those who are also made of dust; and as is the heavenly, such are they also that are heavenly.
49 Kama vile tulivyofanana na yule aliyeumbwa kwa udongo, vivyo hivyo tutafanana na huyohuyo aliyetoka mbinguni.
As we have borne the image of those made of dust, let us also bear the image of the heavenly.
50 Basi, ndugu, nasema hivi: kile kilichofanywa kwa mwili na damu hakiwezi kuushiriki Ufalme wa Mungu; na chenye kuharibika hakiwezi kuwa na hali ya kutoharibika.
Now I say this, brothers, that flesh and blood cannot inherit the Kingdom of God; neither does corruption inherit incorruption.
51 Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa
Look, I tell you a mystery. We will not all sleep, but we will all be changed,
52 wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua. Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza kufa tena, na sisi tutageuzwa.
in a moment, in the twinkling of an eye, at the last trumpet. For the trumpet will sound, and the dead will be raised incorruptible, and we will be changed.
53 Maana ni lazima kila kiharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivalie hali ya kutokufa.
For this corruptible must put on incorruption, and this mortal must put on immortality.
54 Basi, mwili huu wenye kuharibika utakapojivalia hali ya kutoharibika, na kile chenye kufa kitakapojivalia hali ya kutokufa, hapo ndipo litakapotimia lile neno lililoandikwa: “Kifo kimeangamizwa ushindi umekamilika!”
But when this corruptible will have put on incorruption, and this mortal will have put on immortality, then what is written will happen: "Death is swallowed up in victory."
55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Uwezo wako wa kuumiza uko wapi?” (Hadēs )
"Death, where is your victory? Death, where is your sting?" (Hadēs )
56 Ukali wa kifo hutokana na dhambi, nayo dhambi hupata nguvu yake katika Sheria.
The sting of death is sin, and the power of sin is the law.
57 Lakini tumshukuru Mungu anayetupatia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
But thanks be to God, who gives us the victory through our Lord Jesus Christ.
58 Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.
Therefore, my beloved brothers, be steadfast, immovable, always abounding in the Lord's work, because you know that your labor is not in vain in the Lord.