< 1 Wakorintho 12 >
1 Ndugu, kuhusu vipaji vya kiroho, napenda mfahamu vizuri mambo haya:
Now about spiritual gifts, brothers, I do not want you to be uninformed.
2 Mnajua kwamba, kabla ya kuongoka kwenu, mlitawaliwa na kupotoshwa na sanamu tupu.
You know that when you were pagans, you were influenced and led astray to mute idols.
3 Basi, jueni kwamba mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema: “Yesu alaaniwe!” Hali kadhalika, mtu yeyote hawezi kusema: “Yesu ni Bwana,” asipoongozwa na Roho Mtakatifu.
Therefore I inform you that no one who is speaking by the Spirit of God says, “Jesus be cursed,” and no one can say, “Jesus is Lord,” except by the Holy Spirit.
4 Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye ni mmoja.
There are different gifts, but the same Spirit.
5 Kuna namna nyingi za kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.
There are different ministries, but the same Lord.
6 Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote.
There are different ways of working, but the same God works all things in all people.
7 Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote.
Now to each one the manifestation of the Spirit is given for the common good.
8 Roho humpa mmoja ujumbe wa hekima, na mwingine ujumbe wa elimu apendavyo Roho huyohuyo.
To one there is given through the Spirit the message of wisdom, to another the message of knowledge by the same Spirit,
9 Roho huyohuyo humpa mmoja imani, na humpa mwingine kipaji cha kuponya;
to another faith by the same Spirit, to another gifts of healing by that one Spirit,
10 humpa mmoja kipaji cha kufanya miujiza, mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainisha vipaji vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho; humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni, na mwingine kipaji cha kuzifafanua.
to another the working of miracles, to another prophecy, to another distinguishing between spirits, to another speaking in various tongues, and to still another the interpretation of tongues.
11 Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja, ambaye humpa kila mtu kipaji tofauti, kama apendavyo mwenyewe.
All these are the work of one and the same Spirit, who apportions them to each one as He determines.
12 Kama vile mwili ulivyo mmoja wenye viungo vingi, na viungo hivyo vyote—ingawaje ni vingi—hufanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo pia kwa Kristo.
The body is a unit, though it is composed of many parts. And although its parts are many, they all form one body. So it is with Christ.
13 Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwa au watu huru, sote tumebatizwa kwa Roho mmoja katika mwili huo mmoja; na sote tukanyweshwa Roho huyo mmoja.
For in one Spirit we were all baptized into one body, whether Jews or Greeks, slave or free, and we were all given one Spirit to drink.
14 Mwili hauna kiungo kimoja tu, bali una viungo vingi.
For the body does not consist of one part, but of many.
15 Kama mguu ungejisemea: “Kwa kuwa mimi si mkono, basi mimi si mali ya mwili”, je, ungekoma kuwa sehemu ya mwili? La hasha!
If the foot should say, “Because I am not a hand, I do not belong to the body,” that would not make it any less a part of the body.
16 Kama sikio lingejisemea: “Kwa vile mimi si jicho, basi mimi si mali ya mwili”, je, kwa hoja hiyo lingekoma kuwa sehemu ya mwili? La!
And if the ear should say, “Because I am not an eye, I do not belong to the body,” that would not make it any less a part of the body.
17 Kama mwili wote ungekuwa jicho, sikio lingekuwa wapi? Na kama mwili wote ungekuwa sikio, mtu angewezaje kunusa?
If the whole body were an eye, where would the sense of hearing be? If the whole body were an ear, where would the sense of smell be?
18 Lakini kama ilivyo, Mungu alizipanga sehemu hizo tofauti katika mwili kama alivyopenda.
But in fact, God has arranged the members of the body, every one of them, according to His design.
19 Kama sehemu zote zingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
If they were all one part, where would the body be?
20 Ukweli ni kwamba, sehemu za mwili ni nyingi, lakini mwili ni mmoja.
As it is, there are many parts, but one body.
21 Basi, jicho haliwezi kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe”, wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu: “Siwahitaji ninyi.”
The eye cannot say to the hand, “I do not need you.” Nor can the head say to the feet, “I do not need you.”
22 Zaidi ya hayo, inaonekana kwamba sehemu zile za mwili zinazoonekana kuwa ni dhaifu ndizo zilizo muhimu zaidi.
On the contrary, the parts of the body that seem to be weaker are indispensable,
23 Tena, viungo vile tunavyovifikiria kuwa havistahili heshima kubwa, ndivyo tunavyovitunza kwa uangalifu zaidi; viungo vya mwili ambavyo havionekani kuwa vizuri sana, huhifadhiwa zaidi,
and the parts we consider less honorable, we treat with greater honor. And our unpresentable parts are treated with special modesty,
24 ambapo viungo vingine havihitaji kushughulikiwa. Mungu mwenyewe ameuweka mwili katika mpango, akakipa heshima zaidi kiungo kile kilichopungukiwa heshima,
whereas our presentable parts have no such need. But God has composed the body and has given greater honor to the parts that lacked it,
25 ili kusiweko na utengano katika mwili bali viungo vyote vishughulikiane.
so that there should be no division in the body, but that its members should have mutual concern for one another.
26 Kama kiungo kimoja kinaumia viungo vyote huumia pamoja nacho. Kiungo kimoja kikisifiwa viungo vingine vyote hufurahi pamoja nacho.
If one part suffers, every part suffers with it; if one part is honored, every part rejoices with it.
27 Basi, ninyi nyote ni mwili wa Kristo; kila mmoja wenu ni kiungo cha mwili huo.
Now you are the body of Christ, and each of you is a member of it.
28 Mungu ameweka katika kanisa: kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu; kisha ameweka wale wenye kipaji cha kufanya miujiza, kuponya, kusaidia; viongozi na wenye kusema lugha ngeni.
And in the church God has appointed first of all apostles, second prophets, third teachers, then workers of miracles, and those with gifts of healing, helping, administration, and various tongues.
29 Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza?
Are all apostles? Are all prophets? Are all teachers? Do all work miracles?
30 Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha?
Do all have gifts of healing? Do all speak in tongues? Do all interpret?
31 Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonyesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote.
But eagerly desire the greater gifts. And now I will show you the most excellent way.