< 1 Wakorintho 11 >
1 Niigeni mimi kama ninavyomwiga Kristo.
你们应该效法我,一如我效法基督。
2 Nawapeni hongera kwa sababu mnanikumbuka na kwa sababu mnayashikilia yale maagizo niliyowapeni.
我感谢你们时刻记得我,感谢你们始终遵循我向你们宣讲的教义。
3 Lakini napenda pia mjue kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, na mwanamume ni kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo.
但是我希望你们理解,基督是男人的“头”,男人是女人的“头”,上帝是基督的“头。”
4 Basi, kila mwanamume anayesali au anayetangaza ujumbe wa Mungu huku amefunika kichwa chake, huyo anamdharau Kristo.
男人的首领在祈祷或讲道时如果蒙着头,就是羞辱自己的头。
5 Na mwanamke akisali au kutangaza ujumbe wa Mungu bila kufunika kichwa chake, anamdharau mumewe; anayefanya hivyo ni sawa tu na mwanamke aliyenyoa kichwa chake.
女人祷告或讲道时,如果不蒙着头,就是羞辱自己的头,因为这就好比剃发一般。
6 Mwanamke asiyefunika kichwa chake, afadhali anyoe nywele zake. Lakini ni aibu kwa mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa; basi, afadhali afunike kichwa chake.
女人如果没有蒙着头,就应当剪去头发。如果女人以为剪发或剃头很羞耻,就应当蒙着头。
7 Haifai mwanamume kufunika kichwa chake, kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na kioo cha utukufu wake Mungu; lakini mwanamke ni kioo cha utukufu wa mwanamume.
男人不应蒙头,因为他是上帝的形象和荣耀,女人是男人的荣耀。
8 Mwanamume hakutoka kwa mwanamke, ila mwanamke alitoka kwa mwanamume.
因为男人并非来自女人,但女人却来自男人,
9 Mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, ila mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.
男人并非为女人而创造,女人却是为了男人而创造。
10 Ndiyo maana mwanamke hufunika kichwa chake, iwe ishara ya mamlaka yaliyo juu yake, na pia kwa sababu ya malaika.
因此,为了尊重守护天使,女人应当在头上显示权权威记号。
11 Hata hivyo, mbele ya Bwana mwanamke si kitu bila mwanamume, naye mwanamume si kitu bila mwanamke.
尽管如此,从主的角度来看,女人和男人一样重要,男人也和女人一样重要。
12 Kama vile mwanamke alivyotokana na mwanamume, vivyo hivyo mwanamume huzaliwa na mwanamke; kila kitu hutoka kwa Mungu.
正如女人来自男人,男人也来自女人。但更重要的是,万物皆来自上帝。
13 Amueni wenyewe: Je, inafaa mwanamke kumwomba Mungu bila kuvaa kitu kichwani?
你们可以自己判断一下,女人不蒙住头向上帝祷告是否合适?
14 Hata maumbile yenyewe huonyesha wazi kwamba kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu ni aibu kwake mwenyewe;
男人留长发并非自然行为,是一种羞耻。
15 lakini kwa mwanamke kuwa na nywele ni heshima kwake; nywele zake ndefu amepewa ili zimfunike.
但女人留长发却可以给她带来荣耀吗?因为头发就像她的盖头。
16 Kama mtu anataka kuleta ubishi juu ya jambo hili, basi, na ajue kwamba sisi hatuna desturi nyingine, wala makanisa ya Mungu hayana desturi nyingine.
如果有人想要争论这个问题,他们应该意识到,这是教会遵循的唯一习惯。
17 Nikiwa bado nawapeni maagizo haya, siwezi hata kidogo kuwapa ninyi hongera kuhusu haya yafuatayo: mikutano yenu ninyi waumini yaleta hasara zaidi kuliko faida.
我现在做的是指引你们,而非称赞你们,因为当你们聚集在一起,带来的坏处远多于好处。
18 Awali ya yote, nasikia kwamba mnapokutana pamoja hutokea mafarakano kati yenu. Nami naamini kiasi,
首先,我听说你们在聚会的时候起了纷争,我相信这情况属实。
19 maana ni lazima fikira tofauti ziweko miongoni mwenu, ili wale walio thabiti wapate kutambulikana.
你们当然会出现分党结派之事,这样可以真正显示出,那些真诚之人可以真正证明他们自己。
20 Kweli mnakutana, lakini si kwa ajili ya kula chakula cha Bwana!
当你们聚集在一起,你们其实并不是在庆祝主的最后晚餐。
21 Maana mnapokula kila mmoja hukikalia chakula chake mwenyewe, hata hutokea kwamba baadhi yenu wana njaa, na wengine wamelewa!
有人想要先于其他人进餐,让其他人仍然感到饥饿,还有人会喝醉。
22 Je, hamwezi kula na kunywa nyumbani kwenu! Au je, mnalidharau kanisa la Mungu na kuwaaibisha hao wasio na kitu? Niwaambie nini? Niwasifu? La hasha! Si kuhusu jambo hili.
难道你们没有自己的家供你们吃喝吗?还是说,你们藐视上帝的教会,羞辱穷人?我该怎么和你们说呢?夸奖你们做得好吗?你们这样做,我不可能予以称赞。
23 Maana mimi nilipokea kwa Bwana yale maagizo niliyowaachieni: kwamba, usiku ule Bwana Yesu aliotolewa, alitwaa mkate,
我向你们讲述的这一切,都来自主:在主耶稣被出卖的那一夜,他拿起饼,
24 akamshukuru Mungu, akaumega, akasema: “Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka.”
在感谢后便掰开饼,说:“这饼就是我的身体,将赐予你们,你们要这样做来记住我。”
25 Vivyo hivyo, baada ya kula, akatwaa kikombe akasema: “Hiki ni kikombe cha agano jipya linalothibitishwa kwa damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokunywa, kwa kunikumbuka.”
当晚他拿起酒杯,说:“这杯是以我的血订立的新盟约,当你们饮酒的时候要记住我。
26 Maana kila mnapokula mkate huu na kunywa kikombe hiki, mwatangaza kifo cha Bwana, mpaka atakapokuja.
每当你们吃这饼,喝这杯中酒,就是在讲述主的死,直到他回归。”
27 Kwa hiyo, kila aulaye mkate huo au kunywa kikombe cha Bwana bila kustahili, atakuwa na hatia dhidi ya mwili na damu ya Bwana.
因此,任何人如果以不光彩的方式吃主的饼,喝主的杯中酒,就是错对主的身体和主的血,应该感到罪恶感。
28 Basi, kila mtu ajichunguze mwenyewe kwanza, ndipo ale mkate huo na anywe kikombe hicho;
每个人在吃饼和饮这杯中酒时,都应该内省。
29 maana anayekula na kunywa bila kutambua maana ya mwili wa Bwana, anakula na kunywa hukumu yake yeye mwenyewe.
因为吃喝之人如果没有意识到与主身体之间的关系,就会面临审判。
30 Ndiyo maana wengi kati yenu ni dhaifu na wagonjwa, na wengine kadhaa wamekufa.
也是因为这个原因,你们中间有许多人软弱、患病、甚至死去。
31 Kama tungejichunguza wenyewe vizuri hatungeadhibiwa hivyo.
但我们若认真内省,就不会像这样受到审判。
32 Lakini tunapohukumiwa na Bwana, tunafunzwa tuwe na nidhamu, ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
但当我们接受审判时,就是在接受他的管教,以免和世人一起被定罪。
33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana kula chakula cha Bwana, kila mmoja amngoje mwenzake.
所以我的兄弟姐妹们,你们聚集在一起吃下主的最后晚餐,要彼此等待。
34 Na kama kuna yeyote aliye na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kukutana kwenu kusisababishe hukumu. Lakini, kuhusu yale mambo mengine, nitawapeni maelezo nitakapokuja.
如果有人饥饿,应当在家里先吃,免得聚在一起时受到审判。我会在造访你们的时候,给予你们更多的指导。