< Sefania 3 >
1 Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.
这悖逆、污秽、欺压的城有祸了!
2 Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
她不听从命令,不领受训诲, 不倚靠耶和华, 不亲近她的 神。
3 Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
她中间的首领是咆哮的狮子; 她的审判官是晚上的豺狼, 一点食物也不留到早晨。
4 Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
她的先知是虚浮诡诈的人; 她的祭司亵渎圣所, 强解律法。
5 Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.
耶和华在她中间是公义的, 断不做非义的事, 每早晨显明他的公义,无日不然; 只是不义的人不知羞耻。
6 Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
我—耶和华已经除灭列国的民; 他们的城楼毁坏。 我使他们的街道荒凉,以致无人经过; 他们的城邑毁灭,以致无人, 也无居民。
7 Nikasema, 'Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu.' Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
我说:你只要敬畏我,领受训诲; 如此,你的住处不致照我所拟定的除灭。 只是你们从早起来就在一切事上败坏自己。
8 Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
耶和华说:你们要等候我, 直到我兴起掳掠的日子; 因为我已定意招聚列国,聚集列邦, 将我的恼怒—就是我的烈怒都倾在她们身上。 我的忿怒如火,必烧灭全地。
9 Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
那时,我必使万民用清洁的言语 好求告我—耶和华的名, 同心合意地事奉我。
10 Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
祈祷我的,就是我所分散的民, 必从古实河外来,给我献供物。
11 Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
当那日,你必不因你一切得罪我的事自觉羞愧; 因为那时我必从你中间除掉矜夸高傲之辈, 你也不再于我的圣山狂傲。
12 Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
我却要在你中间留下困苦贫寒的民; 他们必投靠我—耶和华的名。
13 Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
以色列所剩下的人必不作罪孽, 不说谎言,口中也没有诡诈的舌头; 而且吃喝躺卧,无人惊吓。
14 Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
锡安的民哪,应当歌唱! 以色列啊,应当欢呼! 耶路撒冷的民哪,应当满心欢喜快乐!
15 Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!
耶和华已经除去你的刑罚, 赶出你的仇敌。 以色列的王—耶和华在你中间; 你必不再惧怕灾祸。
16 Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemi, “Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
当那日,必有话向耶路撒冷说: 不要惧怕!锡安哪; 不要手软!
17 Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
耶和华—你的 神是施行拯救、 大有能力的主。 他在你中间必因你欢欣喜乐, 默然爱你,且因你喜乐而欢呼。
18 katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.
那些属你、为无大会愁烦、 因你担当羞辱的,我必聚集他们。
19 Tazama, Niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, Nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
那时,我必罚办一切苦待你的人, 又拯救你瘸腿的,聚集你被赶出的。 那些在全地受羞辱的, 我必使他们得称赞,有名声。
20 Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, Nitakuwa nimewarudisha”, asema Yahwe.
那时,我必领你们进来,聚集你们; 我使你们被掳之人归回的时候, 就必使你们在地上的万民中有名声,得称赞。 这是耶和华说的。