< Zekaria 2 >

1 Kisha nikainua macho yangu na kuona mtu akiwa na timazi mkononi mwake.
我又舉目觀看,見一人手拿準繩。
2 Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Akaniambia, “Ninakwenda kuupima Yerusalemu ili kujua upana na urefu wake.”
我說:「你往哪裏去?」他對我說:「要去量耶路撒冷,看有多寬多長。」
3 Ndipo malaika aliyekuwa anaongea nami akaondoka na malaika mwingine akaenda kukutana naye.
與我說話的天使去的時候,又有一位天使迎着他來,
4 Malaika wa pili akamwambia, “Nenda uongee na yule kijana umwambie, 'Yerusalemu utakuwa bila kuta kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ndani yake.
對他說:「你跑去告訴那少年人說,耶路撒冷必有人居住,好像無城牆的鄉村,因為人民和牲畜甚多。
5 Kwa maana Yahwe asema, Nitakuwa ulinzi wake, na nitakuwa utukufu katikati yake.
耶和華說:我要作耶路撒冷四圍的火城,並要作其中的榮耀。」
6 Kimbieni! kimbieni! kimbieni kutoka nchi ya kaskazini - asema Yahwe - kwa maana nimewatawanya kama pepo nne za anga! - Asema Yahwe.
耶和華說:「我從前分散你們在天的四方,現在你們要從北方之地逃回。這是耶和華說的。
7 Kimbilieni Sayuni haraka! ninyi mnaokaa na binti Babeli!” Asema Yahwe.
與巴比倫人同住的錫安民哪,應當逃脫。
8 Kwa maana baada ya Yahwe wa majeshi kuniheshimu aliniweka kinyume na mataifa yaliyowateka - kwani awagusaye, agusa mboni ya jicho la Mungu! - baada ya Yahwe kutenda hivi, alisema,
萬軍之耶和華說,在顯出榮耀之後,差遣我去懲罰那擄掠你們的列國,摸你們的就是摸他眼中的瞳人。
9 “Mimi mwenyewe nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka kwa watumwa wao.” Ndipo mtakapojua kwamba Yahwe wa majeshi amenituma.
看哪,我要向他們掄手,他們就必作服事他們之人的擄物,你們便知道萬軍之耶和華差遣我了。
10 “Imba kwa furaha, binti Sayuni, kwa maana mimi mwenyewe nitakaa nawe! - asema Yahwe
錫安城啊,應當歡樂歌唱,因為我來要住在你中間。這是耶和華說的。」
11 Mataifa makubwa yataungana na Yahwe siku hiyo. “Nanyi mtakuwa watu wangu; kwa kuwa nitakaa kati yenu,” nanyi mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.
那時,必有許多國歸附耶和華,作他的子民。他要住在你中間,你就知道萬軍之耶和華差遣我到你那裏去了。
12 Kwa maana Yahwe ataimilki Yuda kama milki yake halali katika nchi takatifu na kwa mara nyingine tena atauchagua Yerusalema kwa ajili yake mwenyewe.
耶和華必收回猶大作他聖地的分,也必再揀選耶路撒冷。
13 Nyamazeni, mbele za Yahwe, ninyi wote wenye mwili, maana ameinuka kutoka mahali patakatifu pake!
凡有血氣的都當在耶和華面前靜默無聲;因為他興起,從聖所出來了。

< Zekaria 2 >