< Zekaria 13 >
1 Katika siku hiyo kijito kitafunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, kwa ajili ya dhambi na uchafu wao.
“那日,必给大卫家和耶路撒冷的居民开一个泉源,洗除罪恶与污秽。”
2 Katika siku hiyo - asema Yahwe wa majeshi - kwamba nitaondoa majina ya sanamu katika nchi ili kwamba yasikumbukwe tena. Nitawaondoa pia katika nchi manabii wa uongo na roho wao mchafu
万军之耶和华说:“那日,我必从地上除灭偶像的名,不再被人记念;也必使这地不再有假先知与污秽的灵。
3 Ikiwa mtu yeyote ataendelea kutoa unabii, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, 'Hautaishi, kwa kuwa umenena uongo kwa jina la Yahwe! Ndipo baba na mama waliomzaa watakapomchoma wakati akitabiri.
若再有人说预言,生他的父母必对他说:‘你不得存活,因为你托耶和华的名说假预言。’生他的父母在他说预言的时候,要将他刺透。
4 Katika siku hiyo kila nabii ataonea aibu maono yake aelekeapo kutoa unabii. Manabii hawa hawatavaa tena vazi la singa, ili kuwadanganya watu.
那日,凡作先知说预言的必因他所论的异象羞愧,不再穿毛衣哄骗人。
5 Kwa maana kila mmoja atasema, 'Mimi siyo nabii! mimi ni mkulima, kwa maana ardhi ndiyo kazi yangu tangu ujana wangu!
他必说:‘我不是先知,我是耕地的;我从幼年作人的奴仆。’
6 Lakini mtu mwingine atamwambia, 'Majeraha haya kati ya mikono yako ni ya nini?' naye atajibu, nilijeruhiwa na waliokuwa katika nyumba ya rafiki zangu.”
必有人问他说:‘你两臂中间是什么伤呢?’他必回答说:‘这是我在亲友家中所受的伤。’”
7 Upanga! inuka mwenyewe dhidi ya mchungaji wangu, mtu asimamaye karibu nami - hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi. Mpige mchungaji, na kondoo watatawanyika! Kwa maana nitageuza mkono wangu dhidi ya wadogo.
万军之耶和华说: 刀剑哪,应当兴起, 攻击我的牧人和我的同伴。 击打牧人,羊就分散; 我必反手加在微小者的身上。
8 Kisha itakuwa kwamba katika nchi yote - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - kwamba theluthi mbili yake itaondolewa! Watu hao wataangamia; theluthi moja tu ndiyo itakayosalia.
耶和华说:这全地的人, 三分之二必剪除而死, 三分之一仍必存留。
9 Nitaipitisha hiyo ya tatu motoni na kuwasafisha kama fedha isafishwavyo; nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo. Wataliitia jina langu nami nitawajibu na kusema, 'Hawa ni watu wangu!' nao watasema, Yahwe ndiye Mungu wangu!”
我要使这三分之一经火, 熬炼他们,如熬炼银子; 试炼他们,如试炼金子。 他们必求告我的名, 我必应允他们。 我要说:这是我的子民。 他们也要说:耶和华是我们的 神。