< Wimbo wa Sulemani 1 >

1 Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Wanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake
שיר השירים אשר לשלמה׃
2 O, laiti ungenibusu na mabasu ya mdomo wako, kwa kuwa upendo wako ni bora kuliko mvinyo.
ישקני מנשיקות פיהו כי טובים דדיך מיין׃
3 Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
לריח שמניך טובים שמן תורק שמך על כן עלמות אהבוך׃
4 Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake nina furuha; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
משכני אחריך נרוצה הביאני המלך חדריו נגילה ונשמחה בך נזכירה דדיך מיין מישרים אהבוך׃
5 Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
שחורה אני ונאוה בנות ירושלם כאהלי קדר כיריעות שלמה׃
6 Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzi wa mashamba ya mizabibu, lakini mshamba langu la mizabibu sijatunza. Wanamke akizungumza na mpenzi wake.
אל תראוני שאני שחרחרת ששזפתני השמש בני אמי נחרו בי שמני נטרה את הכרמים כרמי שלי לא נטרתי׃
7 Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
הגידה לי שאהבה נפשי איכה תרעה איכה תרביץ בצהרים שלמה אהיה כעטיה על עדרי חבריך׃
8 Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
אם לא תדעי לך היפה בנשים צאי לך בעקבי הצאן ורעי את גדיתיך על משכנות הרעים׃
9 Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
לססתי ברכבי פרעה דמיתיך רעיתי׃
10 Mashavu yako ni mazuri na mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
נאוו לחייך בתרים צוארך בחרוזים׃
11 Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
תורי זהב נעשה לך עם נקדות הכסף׃
12 Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu.
עד שהמלך במסבו נרדי נתן ריחו׃
13 Mpenzi wangu ni kwangu kama mkebe wa marashi unao lala usiku katika ya maziwa yangu.
צרור המר דודי לי בין שדי ילין׃
14 Mpenzi wangu ni kwangu kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye
אשכל הכפר דודי לי בכרמי עין גדי׃
15 Ona, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
הנך יפה רעיתי הנך יפה עיניך יונים׃
16 Ona, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi mtanashati.
הנך יפה דודי אף נעים אף ערשנו רעננה׃
17 Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.
קרות בתינו ארזים רחיטנו ברותים׃

< Wimbo wa Sulemani 1 >