< Wimbo wa Sulemani 8 >

1 Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliye nyonya ziwa la mama yangu. Ili kwamba kila ningekuona nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.
Laiti ungelikuwa kwangu kama ndugu wa kiume, ambaye aliyanyonya matiti ya mama yangu! Kisha, kama ningekukuta huko nje, ningelikubusu, wala hakuna mtu yeyote angelinidharau.
2 Nitakuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, na utanifundisha. Nitakupa mvinyo ulio chachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
Ningelikuongoza na kukuleta katika nyumba ya mama yangu, yeye ambaye amenifundisha. Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe, asali ya maua ya mikomamanga yangu.
3 Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kuume unanikumbatia.
4 Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza
Binti za Yerusalemu, ninawaagiza: msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
5 Ni nani huyu anaye kuja kutoka nyikani, amemuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.
Ni nani huyu anayekuja kutoka nyikani akimwegemea mpenzi wake? Mpendwa Nilikuamsha chini ya mtofaa, huko mama yako alipotunga mimba yako, huko yeye alipata utungu akakuzaa.
6 Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote. (Sheol h7585)
Nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri kwenye mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti, wivu wake ni mkatili kama kuzimu. Unachoma kama mwali wa moto, kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa. (Sheol h7585)
7 Maji yalio zuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo, mito haiwezi kuugharikisha. Kama mtu angelitoa mali yote ya nyumbani mwake kwa ajili ya upendo, angelidharauliwa kabisa.
8 Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Nini tutamfanyia dada yetu siku hatakayo ahidiwa kuolewa?
Tunaye dada mdogo, matiti yake hayajakua bado. Tutafanya nini kwa ajili ya dada yetu wakati atakapokuja kuposwa?
9 Kama ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
Kama yeye ni ukuta, tutajenga minara ya fedha juu yake. Na kama yeye ni mlango, tutamzungushia mbao za mierezi.
10 Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
Mimi ni ukuta, nayo matiti yangu ni kama minara. Ndivyo ambavyo nimekuwa machoni pake kama yule anayeleta utoshelevu.
11 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao watalitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.
Solomoni alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-Hamoni; alikodisha shamba lake la mizabibu kwa wapangaji. Kila mmoja angeleta kwa ajili ya matunda yake shekeli 1,000 za fedha.
12 Shamba langu ka mzabibu ni langu, shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanao tunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
Lakini shamba langu la mizabibu ambalo ni langu mwenyewe ni langu kutoa; hizo shekeli 1,000 ni kwa ajili yako, ee Solomoni, na shekeli mia mbili ni kwa ajili ya wale wanaotunza matunda yake.
13 Wewe unaye ishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niweanaye isikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake
Wewe ukaaye bustanini pamoja na marafiki mliohudhuria, hebu nisikie sauti yako!
14 Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.
Njoo, mpenzi wangu, uwe kama swala au kama ayala kijana juu ya milima iliyojaa vikolezo.

< Wimbo wa Sulemani 8 >