< Wimbo wa Sulemani 6 >
1 Mpenzi wako ameenda wapi, ulio mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa njia gani mpenzi wako ameenda? ilitumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
Chorus Quo abiit dilectus tuus, o pulcherrima mulierum? quo declinavit dilectus tuus? et quæremus eum tecum.]
2 Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
[Sponsa Dilectus meus descendit in hortum suum ad areolam aromatum, ut pascatur in hortis, et lilia colligat.
3 Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; na kula katika nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
Ego dilecto meo, et dilectus meus mihi, qui pascitur inter lilia.
4 Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, waamasisha kama jeshi lenye bendera mbele.
Sponsus Pulchra es, amica mea; suavis, et decora sicut Jerusalem; terribilis ut castrorum acies ordinata.
5 Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yana nizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
Averte oculos tuos a me, quia ipsi me avolare fecerunt. Capilli tui sicut grex caprarum quæ apparuerunt de Galaad.
6 Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja aliyefiwa.
Dentes tui sicut grex ovium quæ ascenderunt de lavacro: omnes gemellis fœtibus, et sterilis non est in eis.
7 Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
Sicut cortex mali punici, sic genæ tuæ, absque occultis tuis.
8 Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wadogo bila idadi.
Sexaginta sunt reginæ, et octoginta concubinæ, et adolescentularum non est numerus.
9 Hua wangu, asiye na doa wangu, ni yeye pekee; ni binti muhimu wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wamalikia na masuria walimuona pia, na wakamsifu: Kile walicho sema wamalikia na masuria
Una est columba mea, perfecta mea, una est matris suæ, electa genetrici suæ. Viderunt eam filiæ, et beatissimam prædicaverunt; reginæ et concubinæ, et laudaverunt eam.
10 “Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, ana ng'aa kama jua, uamasisha kama bendera ya jeshi?” Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
Quæ est ista quæ progreditur quasi aurora consurgens, pulchra ut luna, electa ut sol, terribilis ut castrorum acies ordinata?
11 Nimeenda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
Sponsa Descendi in hortum nucum, ut viderem poma convallium, et inspicerem si floruisset vinea, et germinassent mala punica.
12 Nilikuwa nina furaha nikahisi kama nimepakia gari ya farasi la mtoto wa mfalme. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
Nescivi: anima mea conturbavit me, propter quadrigas Aminadab.
13 Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mkamilifu; geuka nyuma, geuka nyuma iliniweze kukushangaa. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katika ya mistari miwili ya wachezaji?
Chorus Revertere, revertere, Sulamitis! revertere, revertere ut intueamur te. Sponsa Quid videbis in Sulamite, nisi choros castrorum?