< Wimbo wa Sulemani 3 >
1 Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye ni mpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.
2 Nilisema binafsi, “Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta.” Nilimtafuta, lakini sikumpata.
Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.
3 Walinzi walinipata walipo kuwa doria katika mji. Nikawauliza, “Mmemuona mpenzi wangu?”
Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?”
4 Ni baada ya mda mfupi kupita nilipo wapita nikampata ninaye mpenda. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipo mleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.
5 Ninataka muape, mabinti wa wanaume waYerusalemu, kwa ayala na paa wa porini, kuwa hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe.
6 Nini hiyo inayo toka nyikani kama nguzo za moshi, umefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote wa manukato unao uzwa na wafanya biashara?
Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani kama nguzo ya moshi, anayenukia manemane na uvumba iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya mfanyabiashara?
7 Angalia, nikitanda cha Sulemani; mashujaa sitini wamekizunguka, wanajeshi elfu sitini wa Israeli
Tazama! Ni gari la Solomoni lisindikizwalo na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli,
8 Wao ni wazoefu wa upanga na wanaujuzi wa vita. Kila mwanaume ana upanga wake pembeni yake, akijizatiti na maasi ya usiku.
wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku.
9 Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.
Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni.
10 Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliekwa dhahabu, na kiti kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo na mabinti wa wanaume wa Yerusalemu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa Yerusalemu
Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu.
11 Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.
Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji, taji ambalo mama yake alimvika siku ya arusi yake, siku ambayo moyo wake ulishangilia.