< Ruth 4 >

1 Ndipo Boazi akaenda kwenye lango la Bethelehemu na kukaa chini. Muda mfupi tu akaja ndugu wa karibu ambaye Boazi alimuongelea. Boazi akamwambia, “Rafiki yangu, njoo hapa na uketi. Kisha mtu huyo akaja na kuketi.
ボアズは町の門のところへ上っていって、そこにすわった。すると、さきにボアズが言った親戚の人が通り過ぎようとしたので、ボアズはその人に言った、「友よ、こちらへきて、ここにおすわりください」。彼はきてすわった。
2 Ndipo Boazi akakusanya viongozi kumi wa mji na kusema, “Katini hapa.” Hivyo wakaketi.
ボアズはまた町の長老十人を招いて言った、「ここにおすわりください」。彼らがすわった時、
3 Boazi alimwambia yule jamaa wa karibu, “Naomi aliyerudi kutoka mji wa Moabu, anauza sehemu ya aridhi ambayo ilikuwa ni miliki ya kaka yetu Elimeleki.
ボアズは親戚の人に言った、「モアブの地から帰ってきたナオミは、われわれの親族エリメレクの地所を売ろうとしています。
4 Nilifikiria kukujulisha na kukwambia, 'Inunue mbele ya hawa waliokaa hapa, na mbele ya viongozi wa watu wangu.' Ikiwa utapenda kuikomboa, ikomboe. Lakini ikiwa hauhitaji kuikomboa, uniambie, ili nijue, kwa kuwa hakuna mwingine wa kuikomboa isipokuwa wewe, na mimi ni mdogo wako.” Ndipo huyo mtu mwingine akasema, “Nitalikomboa.”
それでわたしはそのことをあなたに知らせて、ここにすわっている人々と、民の長老たちの前で、それを買いなさいと、あなたに言おうと思いました。もし、あなたが、それをあがなおうと思われるならば、あがなってください。しかし、あなたがそれをあがなわないならば、わたしにそう言って知らせてください。それをあがなう人は、あなたのほかにはなく、わたしはあなたの次ですから」。彼は言った、「わたしがあがないましょう」。
5 Kisha Boazi akasema, “Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake.”
そこでボアズは言った、「あなたがナオミの手からその地所を買う時には、死んだ者の妻であったモアブの女ルツをも買って、死んだ者の名を起してその嗣業を伝えなければなりません」。
6 Ndipo yule jamaa wa karibu akasema, “Mimi siwezi kuikomboa ardhi kwa ajili yangu bila kuleta athari kwenye urithi wangu binafsi. Nakupa wewe haki ya kuikomboa kwa ajili yako mwenyewe, kwa kuwa mimi sitoweza.”
その親戚の人は言った、「それでは、わたしにはあがなうことができません。そんなことをすれば自分の嗣業をそこないます。あなたがわたしに代って、自分であがなってください。わたしはあがなうことができませんから」。
7 Hii ilikuwa ni desturi ya zamani ya Israeli kuhusu ukombozi na kubadilishana mazuri. Kudhibitisha mambo haya yote, mtu huyu alivua kiatu chake na kumpatia jirani yake; hii ilikuwa ni namna ya kufanya makubaliano ya kisheria katika Israeli.
むかしイスラエルでは、物をあがなう事と、権利の譲渡について、万事を決定する時のならわしはこうであった。すなわち、その人は、自分のくつを脱いで、相手の人に渡した。これがイスラエルでの証明の方法であった。
8 Kwa hiyo huyu jamaa wa karibu akamwambia Boazi, “Inunue mwenyewe.” Kisha akavua kiatu chake.
そこで親戚の人がボアズにむかい「あなたが自分であがないなさい」と言って、そのくつを脱いだので、
9 Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, “Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi.
ボアズは長老たちとすべての民に言った、「あなたがたは、きょう、わたしがエリメレクのすべての物およびキリオンとマロンのすべての物をナオミの手から買いとった事の証人です。
10 Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.”
またわたしはマロンの妻であったモアブの女ルツをも買って、わたしの妻としました。これはあの死んだ者の名を起してその嗣業を伝え、死んだ者の名がその一族から、またその郷里の門から断絶しないようにするためです。きょうあなたがたは、その証人です」。
11 Watu wote na viongozi waliokuwa katika lango, walisema, “Tu mashahidi. Yahweh amfanye mwanamke huyu ambaye amekuja nyumbani kwako kama Raheli na Leya, ambao wawili hawa wameijenga nyumba ya Israeli. Na ubarikiwe katika Efrata na kuwa mashuhuri katika Bethelehem.
すると門にいたすべての民と長老たちは言った、「わたしたちは証人です。どうぞ、主があなたの家にはいる女を、イスラエルの家をたてたラケルとレアのふたりのようにされますよう。どうぞ、あなたがエフラタで富を得、ベツレヘムで名を揚げられますように。
12 Na nyumba yako kama nyumba ya Peres, ambaye Tamari alimzalia yuda, kupitia uzao ambao Yahweh atakupatia pamoja na msichana huyu.”
どうぞ、主がこの若い女によってあなたに賜わる子供により、あなたの家が、かのタマルがユダに産んだペレヅの家のようになりますように」。
13 Hivyo Boazi alimchukua Ruth, na akawa mke wake. Boazi alilala naye, na Yahweh alimruhusu kupata mimba, na alizaa mtoto wa kiume.
こうしてボアズはルツをめとって妻とし、彼女のところにはいった。主は彼女をみごもらせられたので、彼女はひとりの男の子を産んだ。
14 Wanamke huyu akamwambia Naomi, “Yahweh abarikiwe, ambaye hajakuacha bila ndugu wa karibu, yaani mtoto huyu. Jina lake na liwe maarufu katika Israeli.
そのとき、女たちはナオミに言った、「主はほむべきかな、主はあなたを見捨てずに、きょう、あなたにひとりの近親をお授けになりました。どうぞ、その子の名がイスラエルのうちに高く揚げられますように。
15 Na awe kwako mrutubishaji wa maisha na mwenye ruzuku uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa.
彼はあなたのいのちを新たにし、あなたの老年を養う者となるでしょう。あなたを愛するあなたの嫁、七人のむすこにもまさる彼女が彼を産んだのですから」。
16 Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia.
そこでナオミはその子をとり、ふところに置いて、養い育てた。
17 Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Wakawita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi.
近所の女たちは「ナオミに男の子が生れた」と言って、彼に名をつけ、その名をオベデと呼んだ。彼はダビデの父であるエッサイの父となった。
18 Hiki kilikuwa ni kizazi cha Peresi: Peres alimzaa Hezroni,
さてペレヅの子孫は次のとおりである。ペレヅからヘヅロンが生れ、
19 Hezroni akamzaa Ram, Ram akamzaa Aminadabu,
ヘヅロンからラムが生れ、ラムからアミナダブが生れ、
20 Aminadabu akamzaa Nashon, Nashon akamzaa Salmon,
アミナダブからナションが生れ、ナションからサルモンが生れ、
21 Salmon akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obed,
サルモンからボアズが生れ、ボアズからオベデが生れ、
22 Obedi akamzaa Jese, na Jese akamzaa Daudi.
オベデからエッサイが生れ、エッサイからダビデが生れた。

< Ruth 4 >