< Warumi 14 >
1 Mpokeeni yeyote ambaye ni dhaifu katika imani, bila kutoa hukumu kuhusu mawazo yake.
Him that is weak in the faith receive all of you, but not to doubtful disputations.
2 Mtu mmoja ana imani ya kula chochote, mwingine ambaye ni dhaifu anakula mboga tu.
For one believes that he may eat all things: another, who is weak, eats herbs.
3 Mtu ambaye anakula kila kitu asimdharau yeye asiyekula kila kitu. Na yeye ambaye hali kila kitu asimuhukumu mwingine ambaye hula kila kitu. Kwa kuwa Mungu amekwisha mpokea.
Let not him that eats despise him that eats not; and let not him which eats not judge him that eats: for God has received him.
4 Wewe ni nani, wewe ambaye unamuhukumu mtumishi ambaye ni miliki ya mtu mwingine? Ni mbele ya Bwana wake kwamba husimama au huanguka. Lakini atainuliwa, kwa kuwa Bwana anaweza kumfanya asimame.
Who are you that judge another man's servant? to his own master he stands or falls. Yea, he shall be held up: for God is able to make him stand.
5 Mtu mmoja huthamini siku moja kuliko nyingine. Mwingine huthamini kila siku sawa sawa. Hebu kila mtu na ashawishike katika akili yake mwenyewe.
One man esteems one day above another: another esteems every day alike. Let every man be fully persuaded in his own mind.
6 Yeye ambaye anashika siku, anashika kwa ajili ya Bwana. Na kwa yeye alaye, hula kwa ajili ya Bwana, kwa kuwa anampa Mungu shukrani. Yeye ambaye hali, hujizuia kutokula kwa ajili ya Bwana. Yeye pia hutoa shukrani kwa Mungu.
He that regards the day, regards it unto the Lord; and he that regards not the day, to the Lord he does not regard it. He that eats, eats to the Lord, for he gives God thanks; and he that eats not, to the Lord he eats not, and gives God thanks.
7 Kwa kuwa hakuna aishie kwa nafsi yake, na hakuna afae kwa ajili yake mwenyewe.
For none of us lives to himself, and no man dies to himself.
8 Kwa kuwa ikiwa tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na ikiwa tunakufa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi ikiwa tunaishi au tunakufa tu mali ya Bwana.
For whether we live, we live unto the Lord; and whether we die, we die unto the Lord: whether we live therefore, or die, we are the Lord's.
9 Kwa kuwa ni kwa kusudi hili Kristo alikufa na kuishi tena, kwamba awe Bwana wa wote wafu na waishio.
In order to this end Christ both died, and rose, and revived, that he might be Lord both of the dead and living.
10 Lakini wewe, kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe, kwa nini unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
But why do you judge your brother? or why do you set at nothing your brother? for we shall all stand before the judgment seat of Christ.
11 Kwa kuwa imeandikwa, “Kama niishivyo,” asema Bwana, “Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu.”
For it is written, As I live, says the Lord, every knee shall bow to me, and every tongue shall confess to God.
12 Hivyo basi, kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu.
So then every one of us shall give account (logos) of himself to God.
13 Kwa hiyo, tusiendelee tena kuhukumiana, lakini badala yake amua hivi, kwamba hakuna atakaye weka kikwazo au mtego kwa ndugu yake.
Let us not therefore judge one another any more: but judge this rather, that no man put a stumbling block or an occasion to fall in his brother's way.
14 Ninajua na nimeshawishika katika Bwana Yesu, kwamba hakuna kitu kilicho najisi chenyewe. Ni kwa yeye tu anayedhani kuwa chochote ni najisi, kwa kuwa kwake ni najisi.
I know, and am persuaded by the Lord Jesus, that there is nothing unclean of itself: but to him that esteems any thing to be unclean, to him it is unclean.
15 Ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anahuzunika, hautembei tena katika upendo. Usimharibu kwa chakula chako mtu ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa.
But if your brother be grieved with your food, now walk you not charitably. (agape) Destroy not him with your food, for whom Christ died.
16 Hivyo msiruhusu matendo yenu mema yakasababisha watu kuwadhihaki.
Let not then your good be evil spoken of:
17 Kwa kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya chakula na kinywaji, bali ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.
For the kingdom of God is not food and drink; but righteousness, and peace, and joy in the Holy Spirit. (pneuma)
18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo kwa jinsi hii amekubalika kwa Mungu na amekubalika kwa watu.
For he that in these things serves Christ is acceptable to God, and approved of men.
19 Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine.
Let us therefore follow after the things which make for peace, and things wherewith one may edify another.
20 Usiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya chakula. Vitu vyote kwa kweli ni safi, lakini ni vibaya kwa mtu yule ambaye hula na kumsababisha yeye kujikwaa.
For food destroy not the work of God. All things indeed are pure; but it is evil for that man who eats with offence.
21 Ni vyema kutokula nyama, wala kunywa divai, wala chochote ambacho kwa hicho ndugu yako hukwazwa.
It is good neither to eat flesh, nor to drink wine, nor any thing whereby your brother stumbles, or is offended, or is made weak.
22 Hizi imani maalumu ulizo nazo, ziweke kati yako mwenyewe na Mungu. Amebalikiwa yule ambaye hajihukumu mwenyewe katika kile anachokikubali.
Have you faith? have it to yourself before God. Happy is he that condemns not himself in that thing which he allows.
23 Aliye na mashaka amehukumiwa ikiwa anakula, kwa sababu haitokani na imani. Na chochote kisichotokana na imani ni dhambi.
And he that doubts is damned if he eat, because he eats not of faith: for whatsoever is not of faith is sin.