< Ufunuo 9 >
1 Kisha malaika wa tano alipiga tarumbeta yake. Niliona nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka kwenye dunia. Nyota ilipewa ufunguo wa shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho. (Abyssos )
El quinto ángel tocó la trompeta. Vi una estrella que caía del cielo a la tierra. Se le dio la llave del pozo del abismo y (Abyssos )
2 Alifungua shimo lisilo na kikomo, na moshi ukapanda juu kwa safu kutoka ndani ya shimo kama moshi kutoka katika tanuru kubwa. Jua na anga vilibadilika vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka shimoni. (Abyssos )
lo abrió. Del pozo subió un humo, como el de un gran horno. El sol y el aire se oscurecieron a causa del humo del pozo. (Abyssos )
3 Ndani ya moshi nzige walitoka kuja juu ya dunia, nao walipewa nguvu kama ile ya nge juu ya dunia.
Del humo salieron langostas a la tierra, y se les dio poder como el de los escorpiones de la tierra.
4 Waliambiwa kutokudhuru majani katika nchi au mmea wowote wa kijani au mti, isipokuwa tu watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu katika paji za nyuso zao.
Se les dijo que no hicieran daño a la hierba de la tierra, ni a ninguna cosa verde, ni a ningún árbol, sino solo a los hombres que no tienen el sello de Dios en su frente.
5 Hawakupewa ruhusa ya kuwaua hao watu, bali kuwatesa tu kwa miezi mitano. Uchungu wao ulikuwa kama ule wa kuumwa na nge amwumapo mtu.
Se les ordenó que no los mataran, sino que los atormentaran durante cinco meses. Su tormento era como el de escorpión cuando hiere al hombre.
6 Katika siku hizo watu watatafuta kifo, lakini hawatakipata. Watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.
En aquellos días los hombres buscarán la muerte, y de ningún modo la hallarán. Anhelarán morir, y la muerte huirá de ellos.
7 Nzige walifanana na farasi walioandaliwa kwa vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji ya dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
La apariencia de las langostas era semejante a caballos preparados para [la] batalla. Sobre sus cabezas había como coronas que parecían de oro, y sus caras eran como rostros de hombres.
8 Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba.
Tenían cabellos como mujeres, sus dientes eran como de leones,
9 Walikuwa na vifua kama vifua vya chuma na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari mengi ya vita na farasi wakimbiao kwenda vitani.
y tenían corazas como de hierro. El estruendo de sus alas era como el de muchos carruajes de caballos que corren a una batalla.
10 Walikuwa na mikia inayouma kama nge; katika mikia yao walikuwa na nguvu ya kudhuru watu kwa miezi mitano.
Tenían colas semejantes a escorpiones y aguijones. Su poder estaba en sus colas para dañar a los hombres durante cinco meses.
11 Walikuwa naye kama mfalme juu yao malaika wa shimo lisilokuwa na mwisho. Jina lake katika Kiebrania ni Abadoni, na katika Kiyunani ana jina Apolioni. (Abyssos )
Su rey es el ángel del abismo, cuyo nombre en hebreo es Abadón, y en griego Apolión. (Abyssos )
12 Ole ya kwanza imepita. Angalia! Baada ya hili kuna maafa mawili yaja.
El primer ¡ay! pasó. Después de estas cosas vienen aún dos ayes.
13 Malaika wa sita alipiga tarumbeta yake, na nikasikia sauti ikitoka katika pembe ya madhabahu ya dhahabu ambayo iko mbele za Mungu.
El sexto ángel tocó la trompeta. Escuché una voz de los cuernos del altar de oro que estaba delante de Dios,
14 Sauti ilimwambia malaika wa sita aliyekuwa na tarumbeta, “Waachie malaika wanne ambao wamefungwa katika mto mkubwa Efrata.”
la cual decía al sexto ángel que tenía la trompeta: ¡Suelta los cuatro ángeles que están atados junto al gran río Éufrates!
15 Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa kwa saa hiyo maalumu, siku hiyo, mwezi huo, na mwaka huo, waliachiwa wawaue theluthi ya wanadamu.
Fueron desatados los cuatro ángeles que estaban preparados para la hora, día, mes y año, a fin de matar a la tercera parte de los hombres.
16 Idadi ya maaskari waliokuwa juu ya farasi ilikuwa 200, 000, 000. Nilisikia idadi yao.
El número de los jinetes era 200 millones. Escuché su número.
17 Hivi ndivyo nilivyoona farasi katika maono yangu na wale waliopanda juu yao: Vifua vyao vilikuwa vyekundu kama moto, bluu iliyoiva na njano isiyoiva. Vichwa vya farasi vilifanana na vichwa vya simba, na midomoni mwao ulitoka moto, moshi na salfa.
Así vi en la visión los caballos y sus jinetes. Tenían corazas de color fuego, jacinto y azufre. Las cabezas de los caballos eran como cabezas de leones. De sus bocas salían fuego, humo y azufre.
18 Theluthi ya wanadamu waliuawa na haya mapigo matatu: moto, moshi, na salfa iliyotoka katika midomo yao.
Por estas tres plagas, el fuego, el humo y el azufre que salían de sus bocas, murió la tercera parte de los hombres.
19 Kwa kuwa nguvu ya farasi ilikuwa katika midomo yao na katika mikia yao—kwa kuwa mikia yao ilikuwa kama nyoka, na walikuwa na vichwa ambavyo walitumia kuwatia majeraha wanadamu.
El poder de los caballos estaba en sus bocas y en sus colas. Las colas eran semejantes a serpientes con cabezas que dañaban.
20 Watu waliobaki, wale ambao walikuwa hawajauawa na mapigo haya, hawakutubia matendo yao waliyokuwa wamefanya, wala hawakuacha kuabudu mapepo na miungu ya dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti—vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia au kutembea.
El resto de los hombres, los que no murieron por estas plagas, no cambiaron de mente con respecto a las obras de sus manos para no adorar a los demonios y a los ídolos de oro, plata, bronce, piedra y madera, los cuales no pueden ver, ni oír, ni andar.
21 Wala hawakutubia uuaji wao, uchawi wao, uasherati wao au njia zao za wizi.
Tampoco cambiaron de mente con respecto a sus homicidios, ni a sus hechicerías, ni a su inmoralidad sexual, ni a sus robos.