< Ufunuo 7 >

1 Baada ya haya niliona malaika wanne wamesimama kwenye kona nne za dunia, wamezuia pepo nne za nchi kwa nguvu ili kwamba pasiwe na upepo unaovuma katika nchi, juu ya bahari au dhidi ya mti wowote.
And after this I saw four angels standing on the four corners of the earth, holding the four winds of the earth, that the wind should not blow upon the earth, nor the sea, nor upon any tree.
2 Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari:
And I saw another angel coming up from the rising of the sun, having the seal of the living God: and he cried with a great voice to the four angels, to whom it was given unto them to hurt the earth and the sea,
3 “Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu.”
saying, Hurt not the earth, nor the sea, nor the trees, until we may seal the servants of our God in their foreheads.
4 Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144, 000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel:
And I heard the number of the sealed ones: a hundred and forty-four thousand were sealed out of every tribe of the sons of Israel?
5 12, 000 kutoka katika kabila ya Yuda walitiwa muhuri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Rubeni, 12, 000 kutoka katika kabila ya Gadi.
Out of the tribe of Judah twelve thousand were sealed; of the tribe of Reuben twelve thousand; out of the tribe of Gad, twelve thousand;
6 12, 000 kutoka katika kabila ya Asheri, 12, 000 kutoka katika kabila ya Naftali, 12, 000 kutoka katika kabila ya Manase.
of the tribe of Asher, twelve thousand; of the tribe of Napthali, twelve thousand; of the tribe of Manasseh, twelve thousand;
7 12, 000 kutoka kabila ya Simioni, 12, 000 kutoka kabila ya Lawi, 12, 000 kutoka kabila ya Isakari,
of the tribe of Simeon, twelve thousand; of the tribe of Levi, twelve thousand; of the tribe of Issachar, twelve thousand;
8 12, 000 kutoka kabila ya Zebuloni, 12, 000 kutoka kabila ya Yusufu, na 12, 000 kutoka kabila ya Benyamini walitiwa muhuri.
of the tribe of Zebulun, twelve thousand; of the tribe of Joseph, twelve thousand; of the tribe of Benjamin were sealed twelve thousand.
9 Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao,
After these things I saw, and behold a great multitude, which no one was able to number, out of every nation, and tribes, and peoples, and tongues, standing before the throne, and before the Lamb, clothed in white robes, and palms in their hands;
10 na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: “Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!”
and they are crying with a loud voice, saying, Salvation to our God, the one sitting on the throne, and to the Lamb.
11 Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu,
And all the angels stood round about the throne, and the elders, and the four living creatures, and fell down before the throne on their faces, and worshiped God,
12 wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!” (aiōn g165)
saying, Amen: blessing, and glory, and wisdom, and thanksgiving, and honor, and power, and strength, to our God unto the ages of the ages: Amen. (aiōn g165)
13 Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi?
And one of the elders responded, to me saying, Who are these who are clothed in white robes, and whence came they?
14 Nikamwambia, “Bwana mkubwa, unajua wewe,” na akaniambia, “Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.
And I said unto him, My lord, thou knowest. And he said to me; These are those coming up out of great tribulation, who have washed their robes, and made them white in the blood of the Lamb.
15 Kwa sababu hii, wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanamwabudu yeye usiku na mchana katika hekalu lake. Yeye aliye keti juu ya kiti cha enzi atasambaza hema yake juu yao.
On account of this they are before the throne of God, and they worship him day and night in his temple, and the one sitting upon the throne will spread his tabernacle over them.
16 Hawataona njaa tena, wala kiu tena. Jua halitawachoma, wala joto la kuunguza.
And they will never hunger or thirst any more; neither will the sun, or any heat, fall on them:
17 Kwa kuwa Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, na atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima, na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao.”
because the Lamb in the midst of the throne will shepherdize them, and guide them to the fountains of the waters of life; and God will wipe every tear out of their eyes.

< Ufunuo 7 >