< Ufunuo 6 >
1 Nikatazama wakati mwanakondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema kwa sauti iliyofanana na radi, “Njoo!”
2 Nikatazama na palikuwa na farasi mweupe! Aliyempanda alikuwa na bakuli, na akapewa taji. Alitokea kama mshindi ashindaye ili ashinde.
3 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri wa pili, nikasikia mwenye uhai wa pili akisema, “Njoo!”
4 Kisha farasi mwingine akatokea - mwekundu kama moto. Aliye mpanda alipewa ruhusa ya kuondoa amani duniani, ili kwamba watu wachinjane. Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa.
5 Wakati mwanakondoo alipofungua ule muhuri wa tatu, nikasikia mwenye uhai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaona farasi mweusi, na aliyempanda ana mizani mkononi mwake.
6 Nikasikia sauti iliyoonekana kuwa ya mmoja wa wale wenye uhai ikisema, “kibaba cha ngano kwa dinari moja na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiyadhuru mafuta na divai.”
7 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya nne, nilisikia sauti ya mwenye uhai wa nne ikisema, “Njoo!”
8 Kisha nikaona farasi wa kijivu. Aliye mpanda aliitwa jina lake mauti, na kuzimu ilikuwa ikimfuata. Walipewa mamlaka juu ya robo ya nchi, kuua kwa upanga, kwa njaa na kwa ugonjwa, na kwa wanyama wa mwitu katika nchi. (Hadēs )
9 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya tano, niliona chini ya madhabahu roho za wale waliokuwa wameuawa kwa sababu ya neno la Mungu na kutokana na ushuhuda walioushika kwa uthabiti.
10 Wakalia kwa sauti kuu, “mpaka lini, Mtawala wa vyote, mtakatifu na mkweli, utahukumu wakaao juu ya nchi, na kulipiza kisasi damu yetu?”
11 Kisha kila mmoja alipewa kanzu nyeupe na wakaambiwa kuwa wanapaswa kusubiri kidogo hata itakapotimia hesabu kamili ya watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume itakapotimia ambao watauawa, kama vile ambavyo wao waliuawa.
12 Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya sita, nilitazama na palikuwa na tetemeko kuu. Jua likawa jeusi kama gunia la singa, na mwezi mzima ukawa kama damu.
13 Nyota za mbinguni zikaanguka katika nchi, kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga.
14 Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa. Kila mlima na kisiwa vilihamishwa mahali pake.
15 Kisha wafalme wa nchi na watu maarufu na majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mmoja aliye mtumwa na huru, wakajificha katika mapango na katika miamba ya milima.
16 Wakaiambia milima na miamba, “Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo.
17 Kwa kuwa siku kuu ya gadhabu yao imewadia, na ni nani awezaye kusimama?”