< Ufunuo 2 >
1 “Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: 'Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi, “
To the angel of the Church in Ephesus, write. These are the words of Him who holds the seven stars in his right hand, and who walks among the seven golden candlesticks.
2 '“Najua ambacho umetenda na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, na umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.
I know your works and your toil and stedfastness, and that you cannot endure evil men, and that you tested those who called themselves apostles, though they are not, and how you found them false.
3 Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado.
You are holding fast, and have borne up for my names’s sake, and have not grown weary.
4 Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza.
But I have this against you, that you have left your first love.
5 Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.
Remember whence you have fallen, and turn again, and do your first works. Otherwise I am coming to you and will remove your candlestick out of its place, unless you repent.
6 Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia.
But this you have, that you hate the works of the Nicolaitans, which I hate.
7 Kama una sikio, sikiliza yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.'
He who has an ear, let him listen to what the Spirit is saying to the churches. To him that overcomes, to him will I give to eat from the tree of life which is in the garden of God.
8 “Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: 'Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena:
And unto the angel of the Church in Smyrna, write. These are the words of the First and the Last, he who died and has returned to life.
9 '“Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaojiita ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).
I know your persecution and your poverty - but you are rich! I know the reviling of those who say that they themselves are Jews, when they are not, but are a synagogue of Satan.
10 Usiogope mateso yatakayokupata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima.
Fear not what you are about to suffer! Behold, the devil is indeed going to put some of you in prison, that you may be tested, and you will have persecution for ten days. Be faithful even unto death, and I will give you the crown of life.
11 Kama una sikio, sikiliza Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.'
Let him who has ears, listen to what the Spirit is saying to the churches. He that overcomes shall not be hurt of the second death.
12 “Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: 'Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
And to the angel of the Church in Pergamum, write These are the words of Him who holds the sharp two-edged sword.
13 '“Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.
I know where you dwell, where the throne of Satan is; and yet you are holding fast my name, and you have not denied my faith, even in the days of Antipas, my witness, my faithful one, who was slain among you, where Satan has his dwelling.
14 Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israel, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu na kuzini.
But I have a few things against you, because you have there some who hold to the teaching of Balaam, who taught Balak to put a stumbling- block before the sons of Israel, to eat food offered to idols, and to practise immorality.
15 Katika hali iyo hiyo, hata wewe unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.
So you have also some who hold the teaching of the Nicolaitans.
16 Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu.
Repent; if you do not I will very soon come to you, and will make war upon them with the sword of my mouth.
17 Kama una sikio, sikiliza Roho anachowaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya juu ya jiwe, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.'
He who has ears, let him listen to what the Spirit is saying to the churches. To him that overcomes I will give of the hidden manna, and I will give him a white stone, and upon the stone a new name written, which no man knows, but he that receives it.
18 “Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: “Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana:
And to the angel of the Church in Thyatira, write. These are the words of the Son of God, who has his eyes like a flame of fire, and his feet like burnished brass.
19 '“Najua ambacho umefanya - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.
I know your works and your love and faith and service and endurance; I know that your last works are more than the first.
20 Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita mwenyewe nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.
But I have this against you, that you are tolerating that woman Jezebel, who calls herself a prophetess, and she is teaching and leading my slaves astray, leading them to practise immorality, and to eat food which has been sacrificed to idols.
21 Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.
I have given her time for repentance; but she is determined not to turn from her immorality.
22 Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu kwa alichofanya.
Behold, I will lay her on a sick bed, and bring great distress upon those who have committed adultery with her, unless they turn away from her works.
23 Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na tamaa. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.
And moreover, her children will I kill with pestilence. And all the churches shall know that I am he who searches the hearts and souls of men. I will give to each of you according to his works.
24 Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, 'sitaweka juu yenu mzigo wowote.'
But to the rest of you in Thyatira, those who do not hold his teaching, and who do not know the "deep things" of Satan (as they call them),
25 Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.
I say that I am imposing upon you no fresh burden; only hold fast what you have till I come.
26 Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa.
To him that overcomes and perseveres in my works to the end, will I give authority over the nations.
27 'Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.'
And he shall shepherd them with a rod of iron, shattering them like earthen vessels (as I myself have received from my Father),
28 Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi.
and I will give him the Morning Star."
29 Ukiwa na sikio, sikiliza kile ambacho Roho anayaambia makanisa.'
Let him who has an ear, listen to what the Spirit is saying to the churches.