< Ufunuo 15 >
1 Tena nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na yenye kushangaza; Kulikuwa na malaika saba wenye mapigo saba, ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho (katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika).
I saw another great and marvelous sign in the sky: seven angels having the seven last plagues, for in them God's wrath is finished.
2 Niliona kile kilichotokea kuwa bahari ya bilauri iliyochanganywa na moto, na ikasimama pembeni mwa bahari ambapo wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake, na juu ya namba inayowakilisha jina lake. Walikuwa wameshikilia vinubi walivyopewa na Mungu.
I saw something like a sea of glass mixed with fire, and those who overcame the beast, his image, and the number of his name, standing on the sea of glass, having harps of God.
3 Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo: “Kazi zako ni kubwa na zenye kushangaza, Bwana Mungu, utawalaye vyote. Mwaminifu na njia zako ni za kweli, Mfalme wa mataifa.
They sang the song of Moses, the servant of God, and the song of the Lamb, saying, "Great and marvelous are your works, Lord God Almighty. Righteous and true are your ways, King of the nations.
4 Nani atashindwa kukuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu mbele zako kwa sababu u mwema na matendo yako yamejulikana.”
Who would not fear you, Lord, and glorify your name? For you only are holy. For all the nations will come and worship before you. For your righteous acts have been revealed."
5 Baada ya mambo hayo nilitazama, na sehemu takatifu sana, ambapo palikuwa na hema ya ushuhuda, iliyofungukia mbinguni.
After these things I looked, and the temple of the tabernacle of the testimony in heaven was opened.
6 Kutoka mahali patakatifu sana wakaja malaika saba wenye mapigo saba, wamevaa mavazi safi, kitani yenye kung'aa na mshipi wa dhahabu kuzunguka vifua vyao.
The seven angels came out of the temple who had the seven plagues, clothed with pure, bright linen, and wearing golden sashes around their chests.
7 Mmoja wa wale wenye uhai wanne akatoa kwa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu mwenye kuishi milele na milele. (aiōn )
One of the four living creatures gave to the seven angels seven golden bowls full of the wrath of God, who lives forever and ever. (aiōn )
8 Mahali patakatifu sana kulijawa moshi kutoka kwenye utukufu wa Mungu na kutoka kwenye uwezo wake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika.
The temple was filled with smoke from the glory of God, and from his power. No one was able to enter into the temple, until the seven plagues of the seven angels would be finished.