< Ufunuo 13 >

1 Kisha joka alisimama juu ya mchanga ufukwe wa bahari. Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu.
Shesho onzoha ahemeleye pamwanya pesanga mnshenje mnsombi. Shesho nalola omnyama afuma mnsombi. Alina mapeta ilongo na matwe saba. Hu mpeta zyakwe hwali ne taji ilongo, nahwitwe lyakwe hwali nenongwa eyakufulu wa Ngolobhe.
2 Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, na katika kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.
Ono omnyama yehalolile nashi engoya. Amanamagakwe gali nanshi egedobi, nilomu yakwe lyalinanshi elye sama ola onzoha. Wapela enguvu, nahwitengo elyeshimwene, namadalaka ege nguvu sana eya tabhale.
3 Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama.
Hwe elyemnyama omowakwe yabheneshe aje nibhazi igosi lyashele lyenza gasababisye efwa yakwe. Lelo ibhazi lyakwe lyapona nensi yonti yaswiga yafwata omnyama.
4 Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, “Nani kama mnyama? na “Nani atapigana naye?”
Nantele bhaputa onzoha, yani apie amadalaka ola onyama. Bhaputa omnyama nantele, bhendelela ayanje, “Wenu nanshi onyama? na “Wenu yabhakhomane nawo?”
5 Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili.
Onyama wapata ilomu aje ayanje enongwa ezya wizuvwe nendigo aluhusiwe abhe namadalaka humezi amalago gane nazibhele.
6 Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.
Esho omnyama ahiguye ilomlyakwe ayanje endigo hwa Ngolobhe, waliliga itawa lyakwe, ieneo lyashele alikhala nabhala bhabhakhala amwanya.
7 Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa.
Umnyama aluhusiwe alwe na abhelweteshelo nabhamene. Nantele, apete amadalaka pamwanya yashila likabela, na bantu, enjango ni taifa.
8 Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.
Bhonti bhabhakheye mnsi bhaiputa omwene, shila omo yashele itawa lyakwe selisimbilwe, afume abhombwe hunsi, hushitabu eshewomi shashele sha Mwana Ngole, yashele abholilwe.
9 Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize.
Yabha yayonti alini kutu, atejezye.
10 Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.
Nkashele omowakwe ayegwilwe bhatejile nebhema teka abhabhale. Nkashele ome wakwe abhagogwe wipanga, hwipanga abhagogwe. Ohwu wito wapome nagolele nahweteshe hwebho bhabhali bhinza.
11 Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka.
Nantele nalola omnyama ohwamwabho. Ahwenza afume pansi aliwepeta zibhele nashi ilomu nawayanga nashi izoha.
12 Alionyesha mamlaka yote katika mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wakimuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.
Alanjile amadalaka gonti humnyama ola owahwande hwahuhweli hwakwe na abhombe mnsi nabhala bhabhakheye bhali bhahuputa alini bhazi lyakwe lyaliponile.
13 Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu,
Wabhomba amanjele ege nguvu, hata wabhomba omwoto gishe afume amwanya hwitagalila hwa bhantu,
14 na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.
na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.
15 Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe.
Aluhusiwe afumie omwoi walila isanamu lyamnyama aje isanamu ewezye ayanje nasababisye bhala bhonti bhabhakhene apute omnyama bhagogwe.
16 Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso.
Nantele walazimisya shila omo yashele sagali nesamani nabhe ne nguvu, ne nguvu, otajili, nopena yalipalaha nosontezehwo aposhele eshilango hukhono ogwishilume olwenje humonji.
17 Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.
Shali sheshiwezehene hwamtu ahwande olwenje akale hwahulango hwa mnyama, ene namba eya longozezye itawa lyakwe.
18 Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.
Ene ehwanziwa empyana. Aje yoyonti ali no welewa, leshe awezye abhombe embazyo ye namba ya mnyama. Maana namba ya shibhantu. Enamba yakwe yayene 666.

< Ufunuo 13 >