< Zaburi 98 >

1 Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya, kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu; mkono wake wa kuume na mkono wake mtakatifu vimempa ushindi.
מזמור שירו ליהוה שיר חדש כי נפלאות עשה הושיעה לו ימינו וזרוע קדשו׃
2 Yahwe ameufanya wokovu wake ujulikane; ameidhihirisha haki yake kwa mataifa yote.
הודיע יהוה ישועתו לעיני הגוים גלה צדקתו׃
3 Hukumbuka uaminifu wa agano lake na uaminifu kwa ajili ya nyumba ya Israeli; miisho yote ya dunia itauona ushindi wa Mungu wetu.
זכר חסדו ואמונתו לבית ישראל ראו כל אפסי ארץ את ישועת אלהינו׃
4 Mshangilieni Yahwe, nchi yote; pazeni sauti kwa wimbo, imbeni kwa furaha, na imbeni sifa.
הריעו ליהוה כל הארץ פצחו ורננו וזמרו׃
5 Mwimbieni Yahwe sifa kwa kinubi, kwa kinubi na wimbo wenye muiki wa kupendeza.
זמרו ליהוה בכנור בכנור וקול זמרה׃
6 Kwa panda na sauti ya baragumu, fanyeni kelele za shangwe mbele ya Mfalme, Yahwe.
בחצצרות וקול שופר הריעו לפני המלך יהוה׃
7 Bahari na ipige kelele na vyote vilivyomo, ulimwengu na wale wakaao ndani yake!
ירעם הים ומלאו תבל וישבי בה׃
8 Mito na ipige makofi, na milima ipige kelele kwa furaha.
נהרות ימחאו כף יחד הרים ירננו׃
9 Yahwe anakuja kuihukumu nchi; naye ataihukumu dunia kwa haki na mataifa kwa adili.
לפני יהוה כי בא לשפט הארץ ישפט תבל בצדק ועמים במישרים׃

< Zaburi 98 >