< Zaburi 93 >
1 Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa.
Bwana anatawala, amejivika utukufu; Bwana amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa.
2 Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote.
Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwako tangu milele.
3 Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo.
Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.
4 Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu.
Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.
5 Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.
Ee Bwana, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.