< Zaburi 91 >
1 Yeye aishiye katika makazi ya Aliye Juu atakaa katika uvuli wa mwenyezi.
Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nami nitasema kuhusu Yahwe, “Yeye ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye niaamini katika yeye.”
Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”
3 Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti.
Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji, na maradhi ya kuambukiza ya kuua.
4 Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mbawa zake utapata kimbilio, uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.
5 Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana,
6 wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri.
7 Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe.
8 Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu.
9 Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako: naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,
10 Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, hakuna maafa yataikaribia hema yako.
11 Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.
Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote.
12 Nao watakuinua juu kwa mikono yao ili usiweze kujigonga mguu wako kwenye jiwe.
Mikononi mwao watakuinua, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
13 Utawaangamiza simba na nyoka chini ya miguu yako; utawakanyaga wana-simba na nyoka.
Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.
14 Kwa sababu amejitoa kwangu, nitamuokoa. Nitamlinda kwa sababu yeye ni mwaminifu kwangu.
Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa; nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.
15 Aniitapo, nitamjibu. Katika shida nitakuwa naye; nitampatia ushindi na nitamuheshimu.
Ataniita, nami nitamjibu; nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu.
16 Nitamtosheleza kwa maisha malefu na kumuonesha wokovu wangu.
Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu.”