< Zaburi 87 >

1 Mji aliouanzisha umesimama juu ya mlima mtakatifu;
filiis Core psalmus cantici fundamenta eius in montibus sanctis
2 Yahwe anapenda zaidi malango ya Sayuni kuliko mahema yote ya Yakobo.
diligit Dominus portas Sion super omnia tabernacula Iacob
3 Mambo matukufu yamesemwa kwako, mji wa Mungu. (Selah)
gloriosa dicta sunt de te civitas Dei diapsalma
4 Ninataja Rahabu na Babeli kwa wafuasi wangu. Tazama, Filisti, na Tiro, pamoja na Ethiopia nao watasema, 'Huyu alizaliwa humo.'”
memor ero Raab et Babylonis scientibus me ecce alienigenae et Tyrus et populus Aethiopum hii fuerunt illic
5 Itasemwa juu ya Sayuni, “Kila mmoja wa hawa alizaliwa katika yeye; na yeye Aliye Juu atamuimarisha.
numquid Sion dicet homo et homo natus est in ea et ipse fundavit eam Altissimus
6 Yahwe anaandika katika kitabau cha sensa ya mataifa, “Huyu alizaliwa humo.” (Selah)
Dominus narrabit in scriptura populorum et principum horum qui fuerunt in ea diapsalma
7 Hivyo waimbaji na wachezaji kwa pamoja waseme, “chemchem zangu zimo kwako.”
sicut laetantium omnium habitatio in te

< Zaburi 87 >