< Zaburi 84 >
1 Ni jinsi gani maskani yako yapendeza, Ewe Yahwe wa Majeshi!
可拉后裔的诗,交与伶长。用迦特乐器。 万军之耶和华啊, 你的居所何等可爱!
2 Ninashauku ya kuingia nyumbani mwa Yahwe, nimechoka sana kwa sababu ninatamani sana kuwa nyumani mwako. Moyo wangu na mwili wangu wote wakuita wewe Mungu uliye hai.
我羡慕渴想耶和华的院宇; 我的心肠,我的肉体向永生 神呼吁。
3 Hata Shomoro naye amepata nyumba yake na mbayuwayu amejipatia kiota kwa ajili yake mwenyewe mahali awezapo aweza kuweka makinda yake karibu na madhabahu yako, Ee Yahwe wa majeshi, Mfalme wangu, na Mungu wangu.
万军之耶和华—我的王,我的 神啊, 在你祭坛那里,麻雀为自己找着房屋, 燕子为自己找着抱雏之窝。
4 Wamebarikiwa wale ambao huishi katika nyumba yako; nao hukusifu wewe siku zote. (Selah)
如此住在你殿中的便为有福! 他们仍要赞美你。 (细拉)
5 Amebarikiwa mtu yule ambaye nguvu zake ziko katika wewe, katika moyo wake mna njia kuu ziendazo mpaka Sayuni.
靠你有力量、心中想往锡安大道的, 这人便为有福!
6 Wanapopita katika bonde la machozi, hupata chemchem ya maji kwa ajili ya kunywa. Mvua ya vuli hulivika baraka.
他们经过“流泪谷”,叫这谷变为泉源之地; 并有秋雨之福盖满了全谷。
7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu; kila mmoja wao katika sayuni huonekana mbele ya Mungu.
他们行走,力上加力, 各人到锡安朝见 神。
8 Yahwe Mungu wa majeshi, sikia maombi yangu; Mungu wa Yakobo, usikilize nisemacho! (Selah)
耶和华—万军之 神啊,求你听我的祷告! 雅各的 神啊,求你留心听! (细拉)
9 Ee Mungu, uiangalie ngao yetu; uwaangalie wapakwa mafuta wako.
神啊,你是我们的盾牌; 求你垂顾观看你受膏者的面!
10 Kwa maana siku moja katika nyumba yako ni bora kuliko siku elfu mahali pengine. Ni bora niwe mlinzi wa mlango katika nyumba ya Mungu wangu, kuliko kuishi katika mahema ya waovu.
在你的院宇住一日, 胜似在别处住千日; 宁可在我 神殿中看门, 不愿住在恶人的帐棚里。
11 Kwa kuwa Yahwe Mungu ni jua letu na ngao yetu; Yahwe atatoa neema na utukufu; hazuii zuri lolote kwa wale ambao hutembea katika uadilifu.
因为耶和华— 神是日头,是盾牌, 要赐下恩惠和荣耀。 他未尝留下一样好处不给那些行动正直的人。
12 Yahwe wa majeshi, amebarikiwa mtu yule anaye kutumainia wewe.
万军之耶和华啊, 倚靠你的人便为有福!