< Zaburi 77 >
1 Nitampazia Mungu sauti yangu, nitamuita Mungu kwa sauti yangu, na Mungu wangu atanisikia.
エドトンの體にしたがひて伶長にうたはしめたるアサフのうた 我わがこゑをあげて神によばはん われ聲を神にあげなばその耳をわれにかたぶけたまはん
2 Katika siku ya taabu nilimtafuta Bwana; usiku niliinua mikono yangu, nayo haikuchoka. Moyo wangu ulikataa kufarijiwa.
わがなやみの日にわれ主をたづねまつれり 夜わが手をのべてゆるむることなかりき わがたましひは慰めらるるをいなみたり
3 Ningali nikiugua nilielekeza mawazo yangu kwa Mungu. Nilimfikiria Mungu nilipokuwa dhaifu. (Selah)
われ神をおもひいでて打なやむ われ思ひなげきてわが霊魂おとろへぬ (セラ)
4 Uliyafanya macho yangu yasisinzie; nilisumbuka sana kuongea.
なんぢはわが眼をささへて閉がしめたまはず 我はものいふこと能はぬほどに惱みたり
5 Nilifikiri kuhusu siku za kale, kuhusu mambo yaliyopita muda mrefu.
われむかしの日いにしへの年をおもへり
6 Wakati wa usiku niliukumbuka wimbo niliouimba mara moja. Nilifikiria kwa makini na kujaribu kuelewa kile kilichokuwa kimetokea.
われ夜わが歌をむもひいづ 我わが心にてふかくおもひわが霊魂はねもころに尋ねもとむ
7 Je, Mungu atanikataa milele? Je, hatanionesha tena huruma?
主はとこしへに棄たまふや 再びめぐみを垂たまはざるや
8 Je, uaminifu wa agano lake ulikuwa umetoweka milele? Je, ahadi yake imeshindwa milele?
その憐憫はのこりなく永遠にさり そのちかひは世々ながく廃れたるや
9 Je, Mungu amesahau kuwa mwenye neema? Je, hasira yake imeifunga huruma yake? (Selah)
神は恩をほどこすことを忘れたまふや 怒をもてそのあはれみを絨たまふや (セラ)
10 Nilisema, “Hii ni huzuni yangu: mabadiliko ya mkono wa kuume wa Aliye Juu dhidi yetu.”
斯るときに我いへらく此はただわが弱きがゆゑのみいで至上者のみぎの手のもろもろの年をおもひいでん
11 Lakini nitayakumbuka matendo yako, Yahwe; nitafikiri kuhusu matendo yako makuu yaliyopita.
われヤハの作爲をのべとなへん われ往古よりありし汝がくすしきみわざを思ひいたさん
12 Nitayatafakari matendo yako yote nami nitayaishi.
また我なんぢのすべての作爲をおもひいで汝のなしたまへることを深くおもはん
13 Njia yako, Mungu, ni takatifu; ni mungu gani wa kulinganishwa na Mungu wetu aliye mkuu?
紳よなんぢの途はいときよし 神のごとく大なる神はたれぞや
14 Wewe ni Mungu utendaye maajabu; wewe umeonesha nguvu zako kati ya mataifa.
なんぢは奇きみわざをなしたまへる神なり もろもろの民のあひだにその大能をしめし
15 Uliwapa watu wako ushindi kwa uweza wako mkuu - ukoo wa Yakobo na Yusufu. (Selah)
その臂をもてヤコブ、ヨセフの子輩なんぢの民をあがなひたまへり (セラ)
16 Maji yalikuona wewe, Mungu; maji yalikuona wewe, nayo yakaogopa; vina vya maji vilitetemeka.
かみよ大水なんぢを見たり おほみづ汝をみてをののき淵もまたふるへり
17 Mawingu yalitiririsha maji chini; anga zito lilitoa sauti; mishale yako ilipita kati.
雲はみづをそそぎいだし空はひびきをいだし なんぢの矢ははしりいでたり
18 Sauti yako kama ya radi ilisikika katika upepo; radi iliwasha dunia; nchi iliogopa na kutetemeka.
なんぢの雷鳴のこゑは暴風のうちにありき 電光は世をてらし地はふるひうごけり
19 Njia yako ilipita baharini na mapito yako katika maji mengi, lakini alama za miguu yako hazikuonekana.
なんぢの太道は海のなかにあり なんぢの徑はおほみづの中にあり なんぢの蹤跡はたづねがたかりき
20 Uliwaongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Musa na Haruni.
なんぢその民をモーセとアロンとの手によりて羊の群のごとくみちびきたまへり