< Zaburi 76 >

1 Mungu amefanya mwenyewe kujulikana katika Yuda; jina lake ni kuu katika Israeli.
למנצח בנגינת מזמור לאסף שיר ב נודע ביהודה אלהים בישראל גדול שמו
2 Hema yake iko salemu; makao yake yako yako Sayuni.
ויהי בשלם סוכו ומעונתו בציון
3 Huko ndiko alivunja mishale ya upinde, ngao, upanga, na silaha zingine za vita. (Selah)
שמה שבר רשפי-קשת מגן וחרב ומלחמה סלה
4 Wewe unang'aa sana na huufunua utukufu wako, ushukapo kutoka milimani, ambako uliwauwa mateka.
נאור אתה אדיר-- מהררי-טרף
5 Wenye moyo shujaa walitekwa nyara; walilala mauti. Mashujaa wote walikuwa wanyonge.
אשתוללו אבירי לב-- נמו שנתם ולא-מצאו כל-אנשי-חיל ידיהם
6 Kwa kukemea kwako, ewe Mungu wa Yakobo, wote gari na farasi walilala mauti.
מגערתך אלהי יעקב נרדם ורכב וסוס
7 Wewe, ndiyo wewe, ni wa kuogopwa; ni nani awezaye kusimama mbele yako wakati ukiwa na hasira?
אתה נורא אתה--ומי-יעמד לפניך מאז אפך
8 Kutoka mbinguni wewe uliifanya hukumu yako isikike; nchi iliogopa na ikaa kimya
משמים השמעת דין ארץ יראה ושקטה
9 wakati wewe, Mungu, ulipoinuka kutekeleza hukumu na kuwaokoa wote wa nchi walio onewa. (Selah)
בקום-למשפט אלהים-- להושיע כל-ענוי-ארץ סלה
10 Hakika hukumu ya hasira yako dhidi ya binadamu itakuletea wewe sifa; wewe hujifunga mwenyewe hasira yako iliyo baki.
כי-חמת אדם תודך שארית חמת תחגר
11 Wekeni nadhiri kwa Yahwe Mungu wenu na kuzihifadhi. Nao wote wamzungukao yeye mleteeni zawadi yeye ambaye ni wa kuogopwa.
נדרו ושלמו ליהוה אלהיכם כל-סביביו--יבילו שי למורא
12 Yeye huzikata roho za wakuu; huogopwa na wafalme wa nchi.
יבצר רוח נגידים נורא למלכי-ארץ

< Zaburi 76 >