< Zaburi 72 >

1 Mpe mfalme amri ya haki yako, Mungu, haki yako kwa wana wa mfalme.
Zaburi ya Solomoni. Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako.
2 Naye awaamue watu wako kwa haki na maskini wako kwa haki sawa.
Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki.
3 Milima iwazalie watu amani; vilima navyo vizae haki.
Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki.
4 Naye awahukumu watu maskini; awaokoe watoto wa wahitaji na kuwavunja vipande vipande wenye kuwatesa.
Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.
5 Na wakuheshimu wewe wakati wa jua, na kwa kipindi cha kudumu kwa mwezi katika vizazi vyote.
Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
6 Naye apate kuja kama mvua juu ya nyasi zilizokatwa, kama manyuyu yanyunyizayo nchi.
Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7 Mwenye haki na astawi kwa wakati wake, na amani iwepo kwa wingi mpaka mwezi utakapotoweka.
Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8 Na awe na mamlaka toka bahari na bahari, na kutoka Mto hadi miisho ya dunia.
Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.
9 Na wote waishio jangwani wainame mbele zake; adui zake na walambe mavumbi.
Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
10 Wafalme wa Tashishi na visiwa walete kodi; wafalme wa Sheba na Seba watoe zawadi.
Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.
11 Hakika wafalme wote wamwinamie yeye; mataifa yote yamtumikie yeye.
Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
12 Kwa kuwa yeye humsaidia mhitaji na maskini asiye na msaidizi.
Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13 Yeye huwahurumia maskini na wahitaji, na huokoa maisha ya wahitaji.
Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14 Huyaokoa maisha yao dhidi ya mateso na vurugu, na damu yao ni ya thamani machoni pake.
Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
15 Naye apate kuishi! Na dhahabu za Sheba apewe yeye. Watu wamuombee yeye siku zote; Mungu ambariki daima.
Aishi maisha marefu! Na apewe dhahabu ya Sheba. Watu wamwombee daima na kumbariki mchana kutwa.
16 Kuwepo na nafaka nyingi katika ardhi; juu ya milima kuwe na mawimbi ya mimea. Matunda yake yawe kama Lebanoni; watu wasitawi katika miji kama nyansi za kondeni.
Nafaka ijae tele katika nchi yote, juu ya vilele vya vilima na istawi. Tunda lake na listawi kama Lebanoni, listawi kama majani ya kondeni.
17 Jina lake lidumu milele; jina lake ilindelee kama vile jua ling'aavyo; watu wabarikiwe katika yeye; mataifa yote wamwite mbarikiwa.
Jina lake na lidumu milele, na lidumu kama jua. Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake, nao watamwita aliyebarikiwa.
18 Yahwe Mungu, Mungu wa Israel, atukuzwe, ambaye pekee hufanya mambo ya ajabu.
Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa, yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.
19 Jina lake tukufu litukuzawe milele, nayo nchi yote ijazwe na utukufu wake. Amina, Amina.
Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake.
20 Maombi ya Daudi mwana wa Yese yamemalizika. Kutatu cha tatu
Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.

< Zaburi 72 >