< Zaburi 71 >
1 Katika wewe, Yahwe, napatakimbilio salama; usiniache niaibishwe.
耶和华啊,我投靠你; 求你叫我永不羞愧!
2 Uniokoe na kunifanya salama katika haki yako; geuzia sikio lako kwangu.
求你凭你的公义搭救我,救拔我; 侧耳听我,拯救我!
3 Uwe kwagu mwamba kwa ajili ya kimbilio salama ambako naweza kwenda siku zote; wewe umeamuru kuniokoa, kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu.
求你作我常住的磐石; 你已经命定要救我, 因为你是我的岩石,我的山寨。
4 Uniokoe mimi, Mungu wangu, kutoka katika mkono wa asiye haki na katili.
我的 神啊,求你救我脱离恶人的手, 脱离不义和残暴之人的手。
5 Maana wewe ni tumaini langu, Bwana Yahwe. Nimekuamini wewe siku zote tangu nilipokuwa mtoto.
主—耶和华啊,你是我所盼望的; 从我年幼,你是我所倚靠的。
6 Nimekuwa nikisaidiwa na wewe tangu tumboni; wewe ndiye yule uliyenitoa tumboni mwa mama yangu; sifa zangu zitakuhusu wewe siku zote.
我从出母胎被你扶持; 使我出母腹的是你。 我必常常赞美你!
7 Mimi ni mfano bora kwa watu wangu; wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.
许多人以我为怪, 但你是我坚固的避难所。
8 Mama yangu atajawa na sifa zako, siku zote akikuheshimu.
你的赞美,你的荣耀 终日必满了我的口。
9 Usinitupe katika siku za miaka ya uzee wangu; usiniache wakati nguvu zangu zitakapoisha.
我年老的时候,求你不要丢弃我! 我力气衰弱的时候,求你不要离弃我!
10 Maana adui zangu wanazungumza kuhusu mimi; wale wanao fatilia uhai wangu wanapanga njama pamoja.
我的仇敌议论我; 那些窥探要害我命的彼此商议,
11 Wao husema, “Mungu amemuacha; mfuateni na mumchukue, maana hakuna yeyote awezaye kumuokoa yeye.”
说: 神已经离弃他; 我们追赶他,捉拿他吧! 因为没有人搭救。
12 Mungu, usiwe mbali nami; Mungu wangu, harakisha kunisaidia mimi.
神啊,求你不要远离我! 我的 神啊,求你速速帮助我!
13 Waaibishwe na kuharibiwa, wale walio adui wa uhai wangu; wavishwe laumu na kudharauliwa, wale watafutao kuniumiza.
愿那与我性命为敌的,羞愧被灭; 愿那谋害我的,受辱蒙羞。
14 Lakini nitakutumainia wewe siku zote na nitakusifu wewe zaidi na zaidi.
我却要常常盼望, 并要越发赞美你。
15 Kinywa changu kitaongea kuhusu haki yako na wokovu wako mchana kutwa, ingawa ziwezi kuzielewa maana ni nyingi mno.
我的口终日要述说你的公义和你的救恩, 因我不计其数。
16 Nitakuja na matendo yenye nguvu ya Bwana Yahwe; nitataja haki yako, yako pekee.
我要来说主—耶和华大能的事; 我单要提说你的公义。
17 Mungu, tangu ujana wangu wewe umenifundisha; hata sasa ninatangaza matendo yako ya ajabu.
神啊,自我年幼时,你就教训我; 直到如今,我传扬你奇妙的作为。
18 Hakika, hata niwapo mzee na mvi kichwani, Mungu, usiniache mimi, kama ambavyo nimekuwa nikitanga nguvu yako kwa vizazi vijavyo, na uweza wako kwa yeyote ajaye.
神啊,我到年老发白的时候, 求你不要离弃我! 等我将你的能力指示下代, 将你的大能指示后世的人。
19 Pia haki yako, Mungu, iko juu sana; wewe ambaye umefanya mambo makuu, Mungu, ni nani aliye kama wewe?
神啊,你的公义甚高; 行过大事的 神啊,谁能像你!
20 Wewe ambaye umetuonesha sisi mateso mengi utatuhuisha tena na utatupandisha tena juu kutoka kwenye kina cha nchi.
你是叫我们多经历重大急难的, 必使我们复活, 从地的深处救上来。
21 Uiongeze heshima yangu; rudi tena na unifariji.
求你使我越发昌大, 又转来安慰我。
22 Nami pia nitakushukuru kwa kinubi kwa ajili ya uaminifu wako, Mungu wangu; kwako nitaimba sifa kwa kinubi, Mtakatifu wa Israel.
我的 神啊,我要鼓瑟称赞你, 称赞你的诚实! 以色列的圣者啊,我要弹琴歌颂你!
23 Midomo yangu itapiga kelele kwa sababu ya furaha wakati nikikuimbia sifa, hata kwa roho yangu, ambayo wewe umeikomboa.
我歌颂你的时候, 我的嘴唇和你所赎我的灵魂都必欢呼;
24 Ulimi wangu pia utaongea kuhusu haki yangu mchana kutwa; maana wameaibishwa na kuvurugwa, wale waliotafuta kuniumiza.
并且我的舌头必终日讲论你的公义, 因为那些谋害我的人已经蒙羞受辱了。