< Zaburi 70 >
1 Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi.
Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi.
2 Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu.
Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu.
3 Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.”
Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.”
4 Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.”
Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.”
5 Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.
Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.