< Zaburi 7 >
1 Yahweh Mungu wangu, kwako napata kimbilio! Uninusuru na hao wote wanikimbizao, na uniokoe.
Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,
2 Vinginevyo, watanipura kama simba, na kunitawanya viapande vipande na asiwepo mtu wa kuweza kunirudisha katika usalama.
la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa.
3 Yawheh Mungu wangu, Sijawahi kufanya kile maadui zangu wanacho sema nilifanya; sina hatia katika mikono yangu.
Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu,
4 Sijawahi kumkosea mtu yeyote aliye na amani na mimi, au kumdhuru kipumbavu yeyote aliye kinyume na mimi.
au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu,
5 Ikiwa sisemi ukweli basi umruhusu adui yangu kuyaingilia maisha yangu na kuyaharibu; na umuache aukanyage mwili wangu ulio hai kwenye aridhi na kuuacha umelala kwa aibu mavumbini. (Selah)
basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini.
6 Inuka, Yahweh, katika hasira yako; simama kinyume na hasira kali ya adui zangu; amka kwa ajili yangu na ubebe amri zako ambazo wewe umeamuru kwa ajili yao.
Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.
7 Mataifa yote yamekuzunguka; uwatawale kutoka mbinguni.
Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu.
8 Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu.
Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana.
9 Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu.
Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani.
10 Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki.
Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo.
11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anaye chukizwa na waovu kila siku.
Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.
12 Ikiwa kuna mtu hatubu, Mungu atanoa upanga wake na ata andaa upinde wake kwa ajili ya vita.
Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
13 Ana jiandaa kutumia siraha kupambana naye; anatengeneza mishale yake kuwa ya moto.
Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.
14 Fikiria kuhusu huyo ambaye ana ujauzito wa maovu, mwenye mimba ya mipango ya uharibifu, anaye zaa sumu ya uharibifu.
Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
15 Yeye huchimba shimo na kuliacha wazi kisha baadaye hudumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
16 Mipango yake mwenyewe ya uharibifu hugeukia kichwa chake mwenyewe, kwa kuwa vurugu zake mwenyewe humshukia kichwani pake.
Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani.
17 Kwa haki yako Mungu nitakushukuru; nitaimba sifa kwa Mungu aliye juu.
Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.