< Zaburi 67 >

1 Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie (Selah)
למנצח בנגינת מזמור שיר ב אלהים יחננו ויברכנו יאר פניו אתנו סלה
2 ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote.
לדעת בארץ דרכך בכל-גוים ישועתך
3 Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
יודוך עמים אלהים יודוך עמים כלם
4 Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
ישמחו וירננו לאמים כי-תשפט עמים מישר ולאמים בארץ תנחם סלה
5 Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe.
יודוך עמים אלהים יודוך עמים כלם
6 Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki.
ארץ נתנה יבולה יברכנו אלהים אלהינו
7 Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.
יברכנו אלהים וייראו אותו כל-אפסי-ארץ

< Zaburi 67 >