< Zaburi 57 >

1 Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha.
大卫逃避扫罗,藏在洞里。那时,他作这金诗,交与伶长。调用休要毁坏。 神啊,求你怜悯我,怜悯我! 因为我的心投靠你。 我要投靠在你翅膀的荫下, 等到灾害过去。
2 Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu.
我要求告至高的 神, 就是为我成全诸事的 神。
3 Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. (Selah) Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake.
那要吞我的人辱骂我的时候, 神从天上必施恩救我, 也必向我发出慈爱和诚实。
4 Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga.
我的性命在狮子中间; 我躺卧在性如烈火的世人当中。 他们的牙齿是枪、箭; 他们的舌头是快刀。
5 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu, utukufu wako uwe juu ya nchi yote.
神啊,愿你崇高过于诸天! 愿你的荣耀高过全地!
6 Wao walisambaza nje wavu kwa ajili ya miguu yangu; nilikuwa na shida sana. Walichimba shimo mbele yangu. Wao wenyewe wameangukia katikati ya shimo! (Selah)
他们为我的脚设下网罗,压制我的心; 他们在我面前挖了坑,自己反掉在其中。 (细拉)
7 Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa.
神啊,我心坚定,我心坚定; 我要唱诗,我要歌颂!
8 Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri.
我的灵啊,你当醒起! 琴瑟啊,你们当醒起! 我自己要极早醒起!
9 Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa.
主啊,我要在万民中称谢你, 在列邦中歌颂你!
10 Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni.
因为,你的慈爱高及诸天; 你的诚实达到穹苍。
11 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.
神啊,愿你崇高过于诸天! 愿你的荣耀高过全地!

< Zaburi 57 >