< Zaburi 54 >
1 Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu.
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
2 Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu.
Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.
3 Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. (Selah)
Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.
4 Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye.
Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
5 Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu!
Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.
6 Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.
7 Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.
Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.