< Zaburi 51 >

1 Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu.
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kuzini na Bathsheba. Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.
2 Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu.
Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.
3 Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
Kwa maana ninajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.
4 Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.
Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, na kuwa na haki utoapo hukumu.
5 Tazama, nilizaliwa katika uovu; pindi tu mama yangu aliponibeba mimba, nilikuwa katika dhambi. Tazama, wewe unahitaji uaminifu ndani ya moyo wangu;
Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.
6 katika moyo wangu wewe utanifanya niijue hekima.
Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima.
7 Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8 Unifanye kusikia furaha na shangwe ili kwamba mifupa ulioivunja ifurahi.
Unipe kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda na ifurahi.
9 Uufiche uso wako mbali na dhambi zangu na uyafute maovu yangu yote.
Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, na uufute uovu wangu wote.
10 Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
11 Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu.
Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
12 Unirudishie furaha ya wokovu wako, na unihifadhi mimi kwa roho ya utayari.
Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, unipe roho ya utii, ili initegemeze.
13 Ndipo nitawafundisha wakosaji jia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
14 Unisamehe kwa ajili ya umwagaji damu, Mungu wa wokovu wangu, nami nitapiga kelele za shangwe ya haki yako.
Ee Mungu, Mungu uniokoaye, niokoe na hatia ya kumwaga damu, nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.
15 Ee Bwana, uifungue midomo yangu, na mdomo wangu itazieleza sifa zako.
Ee Bwana, fungua midomo yangu, na kinywa changu kitatangaza sifa zako.
16 Kwa maana wewe haufurahishwi katika sadaka, vinginevyo ningekutolea sadaka; wewe hauwi radhi katika sadaka ya kuteketezwa.
Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, hufurahii sadaka za kuteketezwa.
17 Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.
Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.
18 Uitendee mema Sayuni katika nia yako nzuri; uzijenge tena kuta za Yerusalem.
Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.
19 Kisha wewe utafurahia sadaka yenye haki, katika sadaka za kuteketeza; ndipo watu wetu watatoa ng'ombe kwenye madhabahu yako.
Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako.

< Zaburi 51 >