< Zaburi 49 >

1 Sikieni hili, ninyi watu wote; tegeni masikio, ninyi wenyeji wa dunia,
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
2 wote walio chini na walio juu, tajiri na masikini wote pamoja.
Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja:
3 Mdomo wangu utazungumza hekima na tafakari ya moyo wangu itakuwa ya uelewa.
Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
4 Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze:
5 Kwa nini nilazimike kuziogopa siku za uovu, wakati uovu umenizunguka kwenye visigino vyangu?
Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
6 Kwa nini niwaogope wale wanao amini katika mali zao na kujivuna kuhusu utajiri wao?
wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?
7 Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
8 Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha,
9 Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.
10 Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.
11 Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.
12 Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.
13 Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa, .................
Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
14 Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao. (Sheol h7585)
Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. (Sheol h7585)
15 Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. (Selah) (Sheol h7585)
Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. (Sheol h7585)
16 Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.
Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
17 Maana atakapo kufa hataondoka na chochote; utukufu wake hautamfuata yeye.
kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.
18 Yeye huifurahisha nafsi yake awapo hai na watu hukusifu wewe uishipo maisha yako mwenyewe-
Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
19 naye atakwenda kwenye ukoo wa baba zake naye kamwe hataiona nuru tena.
atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.
20 Yule ambaye ana mali lakini hana ufahamu ni kama wanyama, ambao wataangamia.
Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.

< Zaburi 49 >