< Zaburi 49 >
1 Sikieni hili, ninyi watu wote; tegeni masikio, ninyi wenyeji wa dunia,
2 wote walio chini na walio juu, tajiri na masikini wote pamoja.
3 Mdomo wangu utazungumza hekima na tafakari ya moyo wangu itakuwa ya uelewa.
4 Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
5 Kwa nini nilazimike kuziogopa siku za uovu, wakati uovu umenizunguka kwenye visigino vyangu?
6 Kwa nini niwaogope wale wanao amini katika mali zao na kujivuna kuhusu utajiri wao?
7 Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
8 Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
9 Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
10 Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
11 Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
12 Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
13 Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa, .................
14 Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao. (Sheol )
15 Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. (Selah) (Sheol )
16 Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.
17 Maana atakapo kufa hataondoka na chochote; utukufu wake hautamfuata yeye.
18 Yeye huifurahisha nafsi yake awapo hai na watu hukusifu wewe uishipo maisha yako mwenyewe-
19 naye atakwenda kwenye ukoo wa baba zake naye kamwe hataiona nuru tena.
20 Yule ambaye ana mali lakini hana ufahamu ni kama wanyama, ambao wataangamia.