< Zaburi 4 >
1 Unijibu nikuitapo, Mungu wa haki yangu; uniokoe niwapo katika hatari. Unihurumie na usikie maombi yangu.
大卫的诗,交与伶长。用丝弦的乐器。 显我为义的 神啊, 我呼吁的时候,求你应允我! 我在困苦中,你曾使我宽广; 现在求你怜恤我,听我的祷告!
2 Ninyi watu, mpaka lini mtaiabisha heshima yangu? Mpaka lini mtaendelea kupenda kile kisicho stahili na kutafuta uongo?
你们这上流人哪,你们将我的尊荣变为羞辱要到几时呢? 你们喜爱虚妄,寻找虚假,要到几时呢? (细拉)
3 Lakini mjue ya kuwa Yahweh huchagua watu wa kimungu kwa ajili yake. Nitakapo mwita Yahwe atasikia.
你们要知道,耶和华已经分别虔诚人归他自己; 我求告耶和华,他必听我。
4 Tetemekeni na kuogopa, lakini msitende dhambi! Tafakarini mioyoni mwenu kwenye vitanda vyenu na muwe kimya.
你们应当畏惧,不可犯罪; 在床上的时候,要心里思想,并要肃静。 (细拉)
5 Toeni matoleo ya haki na muweke imani yenu katika Yahweh.
当献上公义的祭, 又当倚靠耶和华。
6 Wengi husema, “Ni nani atakaye tuonyesha chochote kilicho kizuri?” Yahweh, utuangazie nuru ya uso wako.
有许多人说:谁能指示我们什么好处? 耶和华啊,求你仰起脸来,光照我们。
7 Umeupa moyo wangu furaha kuu kuliko wao wanapozidishiwa nafaka na divai mpaya.
你使我心里快乐, 胜过那丰收五谷新酒的人。
8 Ni amani kuwa nitajilaza na kusinzia, kwako pekee, Yahweh, nifanye kuwa salama kabisa.
我必安然躺下睡觉, 因为独有你—耶和华使我安然居住。