< Zaburi 34 >

1 Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu.
Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
2 Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi.
Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.
3 Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake.
Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
4 Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.
Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
5 Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
6 Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.
7 Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
8 Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.
9 Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote.
10 Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
11 Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana.
12 Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14 Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.
15 Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.
Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16 Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani.
Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
17 Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.
18 Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.
19 Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
20 Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
21 Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.
Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
22 Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.
Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe.

< Zaburi 34 >