< Zaburi 32 >

1 Zaburi ya Daudi. Zaburi. Amebarikiwa mtu yule aliyesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimesitiriwa.
לדוד משכיל אשרי נשוי-פשע כסוי חטאה
2 Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe hamuhesabii hatia na ambaye rohoni mwake hamna udanganyifu.
אשרי אדם--לא יחשב יהוה לו עון ואין ברוחו רמיה
3 Nilipokaa kimya, mifupa yangu ilidhohofika huku nikiugua muda wote.
כי-החרשתי בלו עצמי-- בשאגתי כל-היום
4 Mchana na usiku mkono wako ulinielemea. nguvu zangu zilikauka wakati wa kiangazi. (Selah)
כי יומם ולילה-- תכבד עלי ידך נהפך לשדי-- בחרבני קיץ סלה
5 Ndipo nilipotambua makosa yangu kwako, nami sifichi tena uovu wangu. Nilisema, “Nitakiri makosa yangu kwa Yahwe,” nawe ulinisamehe hatia ya dhambi zangu. (Selah)
חטאתי אודיעך ועוני לא-כסיתי-- אמרתי אודה עלי פשעי ליהוה ואתה נשאת עון חטאתי סלה
6 Kwa sababu ya haya, wale wote ambao ni wa kimungu wanapaswa kukuomba wakati wa shida kubwa. Nayo mafuriko yajapo, hayatawapata watu hao.
על-זאת יתפלל כל-חסיד אליך-- לעת מצא רק לשטף מים רבים-- אליו לא יגיעו
7 Wewe u mahali pangu pa kujifichia, nawe utanilinda matatizoni. Wewe utanizunguka pamoja na nyimbo zaushindi. (Selah)
אתה סתר לי-- מצר תצרני רני פלט תסובבני סלה
8 Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia upasayo kuiendea. Nitakuelekeza huku macho yangu yakikutazama.
אשכילך ואורך--בדרך-זו תלך איעצה עליך עיני
9 Msiwe kama farasi au kama nyumbu, ambao hawana uelewa; ni kwa hatamu na lijamu tu unaweza kuwapeleka popote utakapo wao waende.
אל-תהיו כסוס כפרד-- אין הבין במתג-ורסן עדיו לבלום בל קרב אליך
10 Waovu wanahuzuni nyingi, bali uaminifu wa agano la Yahwe utamzunguka yule anaye mwamini yeye.
רבים מכאובים לרשע והבוטח ביהוה--חסד יסובבנו
11 Furahini katika Yahwe, na mshangilie, ninyi wenye haki; pigeni kelele za shangwe, ninyi nyote wenye haki mioyoni mwenu.
שמחו ביהוה וגילו צדיקים והרנינו כל-ישרי-לב

< Zaburi 32 >