< Zaburi 25 >

1 Kwako, Yahwe, nayainua maisha yangu!
Zaburi ya Daudi. Kwako wewe, Ee Bwana, nainua nafsi yangu,
2 Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu.
ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda.
3 Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu.
4 Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, nifundishe mapito yako,
5 Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.
niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.
6 Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote.
Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo, kwa maana zimekuwepo tangu zamani.
7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe!
Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala njia zangu za uasi, sawasawa na upendo wako unikumbuke, kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.
8 Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi.
Bwana ni mwema na mwenye adili, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.
9 Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake.
10 Njia zote za Yahwe ni za upendo wa kudumu na niaminifu kwa wote wanao tunza agano na maagizo ya amri zake.
Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.
11 Kwa ajili ya jina lako, Yahwe, unisamehe dhambi zangu, kwa kuwa ni nyingi mno.
Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.
12 Ni nani ambaye anamuogopa Yahwe? Bwana atamfundisha yeye katika njia ambayo anapaswa kuichagua.
Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana? Atamfundisha katika njia atakayoichagua kwa ajili yake.
13 Maisha yake yataenenda katika uzuri; na uzao wake utairithi nchi.
Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, nao wazao wake watairithi nchi.
14 Urafiki wa Yahwe ni kwa ajili ya wale wanao mheshimu yeye, naye hulifanya agano lake lijulikane kwao.
Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake.
15 Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
Macho yangu humwelekea Bwana daima, kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa miguu yangu kutoka mtego.
16 Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.
17 Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
Shida za moyo wangu zimeongezeka, niokoe katika dhiki yangu.
18 Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
Uangalie mateso na shida zangu na uniondolee dhambi zangu zote.
19 Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.
Tazama adui zangu walivyo wengi, pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe; usiniache niaibishwe, Kwa kuwa kwako nakimbilia usalama!
Uyalinde maisha yangu na uniokoe, usiniache niaibike, kwa maana nimekukimbilia wewe.
21 Uadilifu na unyofu vinihifadhi, kwa kuwa nina kutumainia wewe.
Uadilifu na uaminifu vinilinde, kwa sababu tumaini langu ni kwako.
22 Mungu, uiokoe Israeli, na shida yake yote!
Ee Mungu, wakomboe Israeli, katika shida zao zote!

< Zaburi 25 >